**************************
Na John Walter-Babati
Uchaguzi wa ndani wa chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye jumuiya zake ngazi ya wilaya unaendelea leo Septemba 25,2022.
Katika wilaya ya Babati mjini mkoani Manyara takribani kata nane na jumla ya wajumbe 196 wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi kwa lengo la kumchagua Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Ccm ngazi ya wailaya ya Babati Mjini.
Kata zinazounda wailaya ya Babati Mjini ni singe, Bagara ,Mutuka, Bonga Babati, singe, sigino na kata ya Nangara.
Takribani nafasi tisa zinagombewa kupata uongozi mpya wa jumuiya ya wazazi ndani ya wilaya ya Babati Mjini.
Chaguzi za ndani za ccm hufanyika kila baada ya Miaka mitano kama katiba ya Ccm inavyoelekeza ili kudumisha demokrasia na utawala bora.