Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana (Mb), kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 5(1) na 5(4) cha Sheria ya Wakala za Serikali Sura ya 245, amemteua Brigedia Jenerali Mbaraka Naziad Mkeremy kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS). Aidha, amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa hiyo:-
- Dkt. Siima Salome Bakengesa, Mkurugenzi wa Utafiti na Uzalishaji wa Misitu, Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI).
- Eng. Enock Nyanda Emmanuel, Mkurugenzi Msaidizi – Uchumi na Uzalishaji, Ofisi ya Rais TAMISEMI.
- Adv. Piensia Christopher Kiure, Mkurugenzi wa Uhusiano, Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).
- CPA. Bahati Lucas Masila, Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais.
Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 5(5) cha Sheria ya Wakala za Serikali Sura 245, Prof. Dos Santos Aristariki Silayo, Kamishna wa Uhifadhi – TFS, anakuwa Katibu wa Bodi hiyo.
Uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 23 Septemba, 2022 hadi 22 Septemba, 2025