Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akikata utepe kuzindua Kituo cha Mazoezi ya TEHAMA-Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Kongamano la Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) kama Sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 Ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, lililofanyika leo Septemba 23,2022 Jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akipata picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Kituo cha Mazoezi ya TEHAMA-Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Kongamano la Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) kama Sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 Ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, lililofanyika leo Septemba 23,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akisema jambo na Rasi, Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano, Prof. Joel Mtebe katika Kongamano la Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) kama Sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 Ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, lililofanyika leo Septemba 23,2022 Jijini Dar es Salaam. Wadau mbalimbali wa TEHAMA wakiwa katika Kongamano la Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) kama Sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 Ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, lililofanyika leo Septemba 23,2022 Jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akizungumza jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye katika Kongamano la Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) kama Sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 Ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, lililofanyika leo Septemba 23,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akisalimiana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye baada ya kuwasili katika Kongamano la Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) kama Sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 Ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, lililofanyika leo Septemba 23,2022 Jijini Dar es Salaam. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye akizungumza katika Kongamano la Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) kama Sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 Ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, lililofanyika leo Septemba 23,2022 Jijini Dar es Salaam.Rasi, Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano, Prof. Joel Mtebe akizungumza katika Kongamano la Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) kama Sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 Ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, lililofanyika leo Septemba 23,2022 Jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam katika Kongamano la Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) kama Sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 Ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam,lililofanyika leo Septemba 23,2022 Jijini Dar es Salaam.
************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimetakiwa kuangalia uwezekano wa kuongeza idadi ya wahitimu ngazi ya TEHAMA pamoja na kuongeza programu zinazoakisi mahitaji ya soko la ajira na zinazoendana na wakati.
Wito huo umetolewa leo Septemba 23,2022 Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew katika Kongamano la Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) kama Sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 Ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam,
Aidha amesema Ndaki ya TEHAMA ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imefanikiwa kuwapika wahandisi na wanasayansi zaidi ya 50,000 wanaofanya kazi kwenye sekta ya umma na binafsi hivyo basi amewataka waongeze juhudi ili kuongezeka kwa wahitimu kwa awamu nyingine.
Amesema serikali ipo kwenye mchakato wa kuanzisha Taasisi ya TEHAMA itakayokuwa chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari ili kutoa mafunzo maalum na Mahususi katika kada ya TEHAMA.
Hata hivyo amesema kwa mujibu wa taarifa ya Benki ya Dunia ya 2008, kati ya wahitimu milioni 95 wanaohitimu vyuo vikuu, zaidi ya theluthi mbili ya wahitimu hao hawana ujuzi na sifa zinazotakiwa kwenye soko la ajira.
“Hili ni tatizo kubwa sana kwenye vyuo vyetu. Hivyo, basi ni mategemeo yangu kuwa maboresho ya mitaala yanayofanyika katika Ndaki ya TEHAMA yatatoa vijana wenye ujuzi unaohitajika sokoni ikiwa ni pamoja na uwezo wa kufanya bunifu zinazotatua matatizo yetu, kuweza kujiajiri, na kuwaajiri wengine”. Amesema Mhandisi Kundo.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye amesema miaka sitini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salam, Chuo kimeendelea kukua katika udahili wa wanafunzi (shahada za awali na uzamili), vitengo vya kitaaluma, uwezo wa utafiti, programu za kitaaluma, miundombinu, rasilimali watu, huduma za kijamii, sera, na umataifishaji.
“Idadi ya wanafunzi imekuwa ikiongezeka kwa kasi, hadi kufikia 40,885 katika mwaka wa masomo 2020/2021, ambapo wanafunzi wa kike ni asilimia 38 ya wanafunzi wote na juhudi zaidi zimekuwa zikiendelea kuongeza uwiano huu”. Amesema Prof.Anangisye.
Nae Rasi, Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano, Prof. Joel Mtebe amesema pamoja na kwamba mwaka huu Ndaki ya TEHAMA ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imetimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake, historia ya kuanzishwa kwake ni ndefu, iliyokua na mchakato mgumu, na kukabiliana na changamoto nyingi kitaasisi.
Ameeleza kuwa historia ya uanzishwaji wa Ndaki ya TEHAMA imejikita katika jitihada za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kukumbatia, kupanua, na kuimarisha mafunzo, ufundishaji, tafiti, na utoaji wa ushauri wa kutaalamu kwenye eneo la TEHAMA. Hii ikiwa ni pamoja na kujihusisha moja kwa moja na ubunifu, utengenezaji, na uwekaji wa mifumo ya TEHAMA kwa wadau mbalimbali kwenye sekta ya umma na ile ya binafsi ndani na nje ya nchi.