Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa,akizungumza wakati akifungua maadhimisho ya 19 ya siku ya wahandisi nchini yaliyoanza leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Balozi Aisha Amour, akisisitiza jambo kwa wahandisi (hawapo pichani), wakati wa maadhimisho ya 19 ya Siku ya Wahandisi,yaliyoanza leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma.
Msajili wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Bernard Kavishe, akizungumza katika maadhimisho ya 19 ya Siku ya Wahandisi,yaliyoanza leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, akizungumza katika maadhimisho ya 19 ya Siku ya Wahandisi, yaliyoanza leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati akifungua maadhimisho ya 19 ya siku ya wahandisi nchini yaliyoanza leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma.
Wahandisi zaidi ya 200 wakila kiapo cha utii katika maadhimisho ya 19 ya Siku ya Wahandisi,yaliyoanza leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, (aliyevaa koti la blue) akikagua moja ya gari linalotumia umeme asilia lililotengeneza na Chuo cha Teknolojia cha Dar es salaam (DIT), mara baada ya kufungua maadhimisho ya 19 ya siku ya wahandisi nchini,yaliyoanza leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma.
……………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa,amewataka wahandisi nchini kufanya kazi kwa weledi,bidii pamoja na kuzingatia maadili ili kuweza kulisaidia taifa.
Hayo ameyasema leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma wakati akifungua maadhimisho ya 19 ya siku ya wahandisi nchini sambamba na maonyesho ya kazi za wahandisi.
Waziri Mbarawa amesema kuwa kuna miradi mingi ya maendeleo ambayo inatekelezwa hapa nchini,hivyo wahandisi wanapaswa kufanya kazi kwa weledi ili kuendeleza miradi hiyo ya maendeleo.
“Wahandisi ndio nguzo hivyo mnatakiwa muwe na weledi na umakini katika kusimamia miradi ili iwe bora yenye gharama nafuu na inayokamilika kwa muda uliopangwa”, amesema Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake Msajili wa ERB, Mhandisi Bernard Kavishe, amesema kuwa mpaka sasa Bodi imesajili wahandisi 33,773 ambapo kati ya hao wahandisi wanawake ni 4,012 sawa na asilimia 12.98 na kusisitiza Bodi itaendelea kuwaendeleza wahandisi wanawake.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amewataka wahandisi kutekeleza kwa weledi miradi ya maendeleo mkoani Dodoma ili kuzido kuistawisha Makao Makuu.
Maadhimisho ya 19 ya Siku ya Wahandisi yanaongozwa na kauli mbiu “Ubunifu na Uendelezaji wa Ujuzi katika Kuimarisha Maendeleo Endelevu ya Uchumi wa Taifa: Mtazamo wa Kihandisi”.