Naibu Waziri wa Afya,Dk Godwin Mollel,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Umoja wa Wahandisi na Wateknolojia wa Vifaa Tiba Tanzania uliofanyika leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma
Rais wa Umoja wa Wahandisi na Wateknolojia wa Vifaa Tiba Tanzania Mhandisi Valentino Mvanga,akielezea malengo ya Mkutano huo wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Umoja wa Wahandisi na Wateknolojia wa Vifaa Tiba Tanzania uliofanyika leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wahandisi na Wateknolojia wa Vifaa Tiba Tanzania,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Umoja wa Wahandisi na Wateknolojia wa Vifaa Tiba Tanzania uliofanyika leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Huduma za Uchunguzi na HTCTS,Alex Magesa,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Umoja wa Wahandisi na Wateknolojia wa Vifaa Tiba Tanzania uliofanyika leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Wizara ya Afya Paulo Mhame,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Umoja wa Wahandisi na Wateknolojia wa Vifaa Tiba Tanzania uliofanyika leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wafatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Afya,Dk Godwin Mollel (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Umoja wa Wahandisi na Wateknolojia wa Vifaa Tiba Tanzania uliofanyika leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Afya,Dk Godwin Mollel,akipokea Nishani kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan,aliyotunukiwa na Wahandisi na Wateknolojia wa Vifaa Tiba Tanzania kwa kuelekeza fedha nyingi katika teknolojia ya vifaa tiba wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Umoja wa Wahandisi na Wateknolojia wa Vifaa Tiba Tanzania uliofanyika leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Afya,Dk Godwin Mollel,akiwa katika pivha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Umoja wa Wahandisi na Wateknolojia wa Vifaa Tiba Tanzania uliofanyika leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma
……………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
WAHANDISI na Wateknolojia wa Vifaa Tiba Tanzania wamempatia nishani Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza fedha nyingi katika teknolojia ya vifaa tiba.
Akipokea nishani hiyo kwa niaba ya Rais Samia,Naibu Waziri wa Afya,Dk Godwin Mollel amesema hiyo ni heshima kubwa kwa Rais.
Mbali na kupokea nishani hiyo pia Dk.Mollel,amefungua mkutano Mkuu wa mwaka wa Umoja wa Wahandisi na Wateknolojia wa Vifaa Tiba Tanzania uliofanyika leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma
Dk.Mollel amesema Rais Samia amefanya kazi kubwa kwenye sekta ya afya kwa kuwekeza kwenye vifaa tiba.
“Watoto zaidi 500 wametibiwa hapa nchini na kuokoa zaidi ya bilioni 17 ambazo zilitakiwa zitumike kuwapeleka Nje ya Nchi.
Amesema mpaka uchaguzi unakamilika mwaka 2020 ni Hospitali mbili zilikuwa na CT scan lakini kwa sasa Hospitali zote zinaenda kuwa CT Scan.
“Tiba dawa ya mionzi ilikuwa inaenda kuchukuliwa Afrika Kusini lakini leo tuna kiwanda cha kutengeneza mionzi tiba ambayo ipo pale Ocean Road”
“Hayo wenzetu wameyatizama wakasema ni lazima Rais wetu wamshukuru na kumpongeza kwa kazi kubwa.
“Sasa sisi ambacho tunawaomba kwa huu mwaka mmoja amewekeza zaidi ya bilioni 200 kwenye mikono yao wanakazi kubwa ya kusimamia vifaa hivyo,”amesema Naibu Waziri huyo.
Amesema amejiunga kwenye chama hicho kuhakikisha vifaa tiba vinatunzwa pamoja kupunguza gharama za kutibu.
Hata hivyo,Dk.Mollel amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Hospitali za Taifa, Kanda,Mikoa na Wilaya wahakikishe wanapofanya manunuzi yoyote ya vifaa tiba ni lazima wataalamu wa Vifaa tiba washirikishwe.
Amesema hata Wizara ya Afya wakati mwingine vinaponunuliwa vifaa tiba anasimamia mtaalamu wa maabara,washirikiane ili ubora upatikane.
“Tukikuta vifaa vimenunuliwa na wataalamu hawajashirikishwa hilo ni tatizo msikae nyuma simamieni eneo lenu,”amesema Dk.Mollel.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Huduma za Uchunguzi na HTCTS,Alex Magesa amesema wanaomba kuunda Bodi ya taaluma ya vifaa tiba.
Amesema kupitia Bodi hiyo watahakikisha mambo yanaenda vizuri na juhudi zinaendelea kuengeza idadi ya waajiriwa.
“Tunajua mna uchache wa karakana za kuhudumia vifaa vyetu na kwa Sasa zipo katika maeneo machache.
Amesema Serikali inajitahidi kuhakikisha kazi zinazotendeka zinafanyika kwa mujibu wa muongozo.
Amesema miongozo inatekelezwa pale kunapokuwa na watu wa kutosha ili iweze kutumia vizuri.
“Tunategemea miongozo hiyo itatengenezwa na kuhuishwa ili huduma zetu ziwe sahihi,”amesema
Amesema wataendelea kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kitaaluma kunaboreshwa na kimaslahi.