Mkufunzi wa uhandisi Matengenezo ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Castory Njako,akizungumza na waandishi wa habari katika banda la chuo hicho wakati wa maadhimisho ya 19 ya siku ya wahandisi nchini yanayoendelea jijini Dodoma.
………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
CHUO Cha Taifa Cha Biashara (NIT) kimewaita watanzania kuangalia project mbalimbali ambazo wanafunzi wamezibuni katika chuo hicho katika banda lao.
Hayo yamesemwa leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma Mkufunzi wa uhandisi Matengenezo ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Castory Njako katika banda la chuo hicho wakati wa maadhimisho ya 19 ya siku ya wahandisi nchini
Bw. Njako amesema kuwa kuna project mbalimbali za wanafunzi ambao wamezifanya.
Amesema project hizo zimetokana na wanafunzi waliohitimu katika idara ya uhandisi wa ndege, mitambo na fani mbalimbali.
Amesema kwa kawaida wanafunzi wanaanza na nadharia kwa walimu kuingia darasani wanafundisha na baada ya hapo wanafunzi huwa wamepata ujuzi.
“Hapa tunaunga vitu mbalimbali kuna project ya kutengeneza mguu wa ndege na mashine ya kuoshea magari unaingiza chafu inatoka safi.Kuna project wauza maziwa unaingiza sarafu unapata maziwa,”amesema.
Kwa upande wake,mwanafunzi aliyemaliza katika chuo hicho,Hellen Ignatius ambaye amebuni kifaa cha kuoshea gari amesema alipata wazo la kubuni kifaa hicho mara baada ya kuona unatumika muda mrefu kuosha gari.
Amesema lengo la kifaa hicho ni magari yamekuwa mengi na muda unaotumika kuoshea gari moja ni mwingi hivyo kutumia kifaa hicho kitasaidia kuokoa muda na maji.
“Stage ya kwanza ni kwa ajili maji masafi,stage ya pili ni sabuni na stage ya tatu ni kuliweka safi na kukausha,”amesema.