MKURUNGEZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) Mhandisi Modestus Lumato,akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya 19 ya siku ya wahandisi nchini yanayoendelea jijini Dodoma.
MKURUNGEZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) Mhandisi Modestus Lumato,akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya 19 ya siku ya wahandisi nchini yanayoendelea jijini Dodoma.
……………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
MKURUNGEZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) Mhandisi Modestus Lumato,ameeleza kuwa idadi ya watu wanaobadili magari kutoka katika matumizi ya mafuta na kuingia katika gesi inaongezeka kwa kasi.
Hayo ameyasema wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya 19 ya siku ya wahandisi nchini yanayoendelea jijini Dodoma.
Mhandisi Lumato,amesema kuwa kwa sasa wanaendelea kuhimiza wawekezaji kuongeza kujenga idadi ya vituo vya kujazia gesi ili kuendana na kasi hiyo.
“Watu wamehamsika kwa kasi sana kubadilisha magari yao kutoka katika matumizi ya mafuta na kuhamia katika matumizi ya gesi EWURA kwa sasa tunaendelea kuhimiza wawekezaji wote waweze kujenga vituo vya kutosha ili kukidhi mahitaji ya ongezeko hilo.”amesema Mhandisi Lumato
Aidha amesema kuwa kwasasa kuna vituo vutatu vya kujazia gesi katika magari ambavyo ni ubungo, TAZARA na Mtwara.
Kuhusu kupanda kwa bei za mafuta Mhandisi Lumato amesema ni tatizo la kidunia sio Tanzania pekee ambapo kila nchi inahangaika kwa namna yake jinsi inavyoweza kuokoa wananchi wake.
Mhandisi Lumato amesema kwa Tanzania Rais Samia anaendelea kuhangaika ili kuhakikisha anapunguza kasi ya ongezeko la bei kwa kutoa fedha sh.milion 100 kila mwezi ilio kupunguza makali ya bei.
“Tunaendelea na utaratibu wa kuhamasisha watu waweze kubadilisha magari yao ili waweze kutumia gesi ambayo imeonekana ni rahisi na kwa asilimia 70 ni salama,”