Kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kumteua Dkt. Oswald Jotam Masebo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Makumbusho ya Taifa la Tanzania (NMT), Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana (Mb) kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 4(1)-(2) cha Sheria ya Makumbusho ya Taifa ya Mwaka 1980, amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Makumbusho ya Taifa la Tanzania (NMT):-
1. Prof. Thomas Jacob Lyimo, Rasi wa Ndaki ya Sayansi Asilia na Tumizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
2. Dkt. Mboni Amiri Ruzegea, Mkurugenzi Mkuu, Maktaba ya Taifa Dar es Salaam.
3. Bw. Said Habibu Tunda, Meneja wa Uwekezaji, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Dar es Salaam.
4. Bi. Mystica Mapunda Ngongi, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Dar es Salaam.
5. Bw. Asangye Nicholas Bangu, Kaimu Mtendaji Mkuu, Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, Dar es Salaam.
6. Bw. Alpha A. S. Zullu, Meneja Rasilimaliwatu na Utawala, Baraza la Mitihani la Taifa Tanzania (NECTA).
Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 4(2) cha Sheria hiyo, kikisomwa kwa pamoja na Jedwali la Kwanza, Kipengele Na.1(1)(b) Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania (NMT), Dkt. Noel Biseko Lwoga anakuwa Katibu wa Bodi hiyo.
Uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 21 Septemba, 2022 hadi 20 Septemba, 2025.