Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Wabunge kutoka Bunge la Zimbabwe ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Afya na Huduma kwa Watoto kutoka Bunge hilo wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kanali Mstaafu Dkt. Joshua Murire (kulia) katika kikao kilichofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimpatia zawadi yenye mfano wa jengo la Bunge, Mbunge kutoka Bunge la Zimbabwe ambae pia ni Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Afya na Huduma kwa Watoto, Kanali Mstaafu Dkt. Joshua Murire pale ugeni kutoka Bunge hilo ulipomtembelea leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge kutoka Bunge la Zimbabwe ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Afya na Huduma kwa Watoto wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kanali Mstaafu Dkt. Joshua Murire (kulia kwake) baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)