*************************
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Sept 20
KATIBU Tawala mkoa wa Pwani,Zuwena Omary amekemea Mashirika yasiyo ya kiserikali ya mikononi ,mifukoni na yale ya kifamilia ambayo yamekuwa yakijinufaisha yenyewe na badala yake yajikite kutekeleze wajibu wao kwa mujibu wa usajili .
Aidha ametoa maelekezo kwa Mashirika hayo ,kudumisha mawasiliano na Serikali kwa kutoa taarifa zao za utekelezaji zenye uwazi na sahihi .
Akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2021,ulioandaliwa na ofisi ya Mkuu wa mkoa huo, na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka mashirika 45 ,alieleza ni wajibu wao kufuata sheria na kanuni ili kuepuka kutumika vibaya.
“Unakuta Shirika kila mwaka halina ofisi,wanatafuta ofisi kila mwaka ,ukiwahitaji kuwapata kwao hadi kwenye simu, sitopenda kusikia kuna Shirika lisilo la kiserikali la mkononi,mfukoni na yale ya kifamilia yaliyoanzishwa kwa manufaa yao,”Tukiwahitaji tujue ofisi zilipo na mnapatikana wapi”alisisitiza Zuwena.
“Kwa taarifa zilizopo kuna Mashirika yaliyosajiliwa kufanya kazi kimkoa 303 ,kati ya haya 82 hayafanyi kazi,yalianza Lakini yamekwama,Hapa Lazima tujitafakuri kwanini hatufikii malengo”
“Yapo pia ambayo yanajihusisha na masuala ya madawa ya kulevya, watoto, wanawake,vijana ,ustawi wa jamii na afya Lakini hawafikiwi, unakuta wapo wengi wanahitaji msaada ,na shauri kuwafikia ambao hawajafikiwa”alifafanua Zuwena.
Nae Msajili Msaidizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani hapo, Kissaga Mgeni alisema , mkoa una mashirika hayo 303 kati ya hayo 82 ndio yapo hai ikiwa ni sawa na asilimia 27.1, miradi iliyotekelezwa ni 104 yenye thamani ya sh.bilioni 1.6 huku wanufaika wakiwa 163,826.
Mjumbe kutoka Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali akiwakilisha mkoa wa Pwani, Gaidon Haule alitaja changamoto zinazowakabili ,ikiwemo Ukosefu wa elimu katika Uelewa wa miongozo na sheria sahihi na kanuni juu ya sekta hiyo hali inayosababisha kufungiwa na wengine Kuwa na madeni makubwa ya Mamlaka ya mapato , sanjali na kushindwa kujiendeleza baada ya wafadhili kusitisha ufadhili.