Katibu Mkuu wa chama cha Wafanyakazi RAAWU Joseph Sayo akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wanachama juu ya kukuza mahusiano bora mahala pa kazi
Mratibu wa mafunzo kutoka RAAWU Mariam Mgalula ,akizungumza kwenye semina itakayodumu kwa siku tano Jijini Mwanza.
Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa chama cha Wafanyakazi RAAWU
…………………………………………
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Chama cha Wafanyakazi (RAAWU) kimeandaa mafunzo maalumu kwaajili ya kuwajengea uwezo wananchama juu ya kukuza mahusiano bora mahala pa kazi.
Semina hiyo itakayodumu kwa siku tano inafayika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwanza Hotel.
Akizungumza wakati wa kufungua semina Katibu Mkuu wa RAAWU Taifa Joseph Sayo, alisema wamekutana kwaajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na sheria za kazi ikiwemo sheria namba 6,8 ambazo zote zinawahusu watumishi wa umma na sekta binafsi ili baada ya mafunzo hayo viongozi wa matawi na menejimenti wawe na uelewa unaofanana kuhusu namna bora ya kutekeleza sheria za kazi hatua itakayosaidia kuondoa migongano ya uelewa.
Sayo alitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa washiriki wa mafunzo hayo kushiriki kikamilifu katika mada mbalimbali ambazo zitatolewa ikiwemo ya Haki kodi ambayo itawasaidia kujua nikwanamna gani Kodi zao zinatumika Serikalini kwaajili ya kuleta maendeleo.
Mratibu wa mafunzo kutoka RAAWU Mariam Mgalula,alisema katika mafunzo hayo watakuwa na mada tano ambazo ni Mifuko ya hifadhi ya jamii, mabadiliko ya tabianchi,Haki kodi, ujasiriamali pamoja na sheria za kazi.
Alisema anategemea baada ya mafunzo hayo waajiri na wawakilishi wa waajiri wataondoka na vitu vingi ambavyo vitawasaidia kutoa elimu kwenye matawi yao.
“Baada ya mafunzo haya wanaporudi kwenye matawi yao hata kama kunatatizo litatokea watakuwa wepesi kulitatua hatua itakayosaidia chama cha Wafanyakazi RAAWU kupata wepesi wa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi kuanzia ngazi za matawi”, alisema Mgalula
Kwa upande wake Mwenyekiti wa RAAWU Kanda ya ziwa Dkt.Denna Michael, alisema mafunzo hayo yatawasaidia waajiri, viongozi wa chama cha Wafanyakazi RAAWU nchi nzima kujadili mambo mahususi yanayohusu sheria za kazi pamoja na kujifunza sheria mpya ya mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuweza kupata uelewa wa pamoja ambao utaleta tija kwenye taasisi mbalimbali.
Naye Afisa rasilimali watu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mariam Mbarouk,alisema mafunzo hayo yatamsaidia kuwa na hoja zenye tija za kujadili pindi atakapokutana na vyama vya wafanyakazi huku akitoa wito kwa wafanyakazi kuendelea kutimiza wajibu wao kikamilifu.