***********************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:
- Amemteua Prof. Mohamed Yakubi Janabi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili. Prof. Janabi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Prof. Janabi anachukua nafasi ya Prof. Lawrence Maseru ambaye amestaafu.
- Amemteua Dkt. Peter R. Kisenge kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Dkt. Kisenge anachukua nafasi ya Prof. Janabi. Dkt. Kisenge ni Mkurugenzi wa Tafiti na Mafunzo wa (JKCI).
Uteuzi huu umeanza tarehe 02 Oktoba, 2022.