Waziri wa Maji Jumaa Aweso,akizungumza na washiriki mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu (WSDP III) hafla iliyofanyika leo Septemba 16,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu (WSDP III) hafla iliyofanyika leo Septemba 16,2022 jijini Dodoma.
MWAKILISHI wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.Saitore Laizer,akiipongeza wizara ya maji kwa kushirikiana na Wizara ya Afya wakati wa uzinduzi wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu (WSDP III) hafla iliyofanyika leo Septemba 16,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa uzinduzi wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu (WSDP III) hafla iliyofanyika leo Septemba 16,2022 jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Wadau wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia Bi. Ruth Walker, ameipongeza serikali kwa jitihada zinazofanyika kuhakikisha changamoto za upatikanaji wa majisafi na salama zinapatiwa ufumbuzi wakati wa uzinduzi wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu (WSDP III) hafla iliyofanyika leo Septemba 16,2022 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji Dkt.Christine Ishengoma ,akitoa salamu za Kamati yake wakati wa uzinduzi wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu (WSDP III) hafla iliyofanyika leo Septemba 16,2022 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Asasi za Kiraia (CSOs) Herbert Kashililala,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu (WSDP III) hafla iliyofanyika leo Septemba 16,2022 jijini Dodoma.
MKUU wa Kitengo cha Uratibu Wizara ya Maji Bw.Remigius Mazigwa akitoa taarifa kuhusu WSDP III wakati wa uzinduzi wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu (WSDP III) hafla iliyofanyika leo Septemba 16,2022 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu (WSDP III) hafla iliyofanyika leo Septemba 16,2022 jijini Dodoma.
MWAKILISHI wa Katibu Mkuu TAMISEMI Bi.Martha Mariki,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu (WSDP III) hafla iliyofanyika leo Septemba 16,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Maji Jumaa Aweso (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu (WSDP III) hafla iliyofanyika leo Septemba 16,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso,akiwa na viongozi pamoja na wadau wa Maji wakizindua Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu (WSDP III) hafla iliyofanyika leo Septemba 16,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso,akizungumza na washiriki mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu (WSDP III) hafla iliyofanyika leo Septemba 16,2022 jijini Dodoma.
…………………………
Na.Alex Sonna-DODOMA
WIZARA ya Maji inatarajia kutumia takribani Dola za Kimarekani Sh. bilioni 6.46 kutekeleza Awamu ya Tatu ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji iliyoanza Julai 2022 hadi Juni 2026 ili kufikia maendeleo endelevu ya usimamizi wa rasilimali za maji hapa nchini
Hayo yamesemwa leo Septemba 16,2022 jijini Dodoma na Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakati wa uzinduzi wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya tatu (WSDP III).
”Gharama ya utekelezaji wa Programu hiyo inakadiriwa kuwa Dola za Marekani Bilioni 6.46 na inalenga kufanikisha utekelezaji wa miradi ya usimamizi na uendelezaji rasilimali za maji, upatikanaji wa majisafi na salama na miradi ya usafi wa mazingira hapa nchini. ”amesema Aweso
Aidha amesema kuwa utekelezaji wa Awamu ya kwanza ulianza Julai 2009 na kumalizika Juni 2016, Awamu ya pili ilianza Julai 2016 na kumalizika Juni 2022 na Awamu ya tatu na ya mwisho imeanza kutekelezwa Julai 2022 na itakamilika 2026.
“Madhumuni ya Maendeleo ya Programu ni Kuimarisha Taasisi za Kisekta kwa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Maji, Ubora wa Maji, Kuboresha Upatikanaji wa Huduma za Majisafi na Usafi wa Mazingira,”amesema Aweso.
Amesema kuwa baada ya kukamilika kwa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji Awamu ya Kwanza na ya Pili, Wizara inajivunia mafanikio makubwa katika Sekta ya Maji ikiwa ni pamoja na maboresho katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji ikiwemo kuanzishwa kwa Bodi tisa za Maji za Mabonde, maabara 7 kati ya 17 za Ubora wa Maji kupewa vyeti vya Ithibati, kuimarika kwa kiwango cha huduma ya maji vijijini hadi kufikia asilimia 72.3.
Hata hivyo amezitaka Asasi za Kiraia (AZAKI) na wadau wote wa Sekta ya Maji kuendelea kushirikiana na Sekta ya Maji ambayo ni muhimu katika kuinua uchumi wa jamii nchini.
“Nawashukuru sana kwa kujitokeza kwa sababu uwepo wenu katika hafla hii kunaonyesha dhamira yenu ya dhati ya kuendelea kushirikiana na Sekta ya Maji katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi, salama na ya uhakika. Niwaombe tuendeleze ushirikiano huu ili tuyafikie kwa pamoja malengo tuliyojiwekea” Waziri Aweso amesema.
Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amesema kuwa programu hiyo inalenga katika kufikia asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini ya wananchi wanaopata huduma ya maji safi na salama ifikapo 2025.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Wadau wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia Bi. Ruth Walker ameipongeza serikali kwa jitihada zinazofanyika kuhakikisha changamoto za upatikanaji wa majisafi na salama zinapatiwa ufumbuzi. Amesema Benki ya Dunia iko tayari kuendeleza ushirikiano huo.
Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Dkt. Saitore Laizer amesema program hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza magonjwa ya mlipuko, kuongeza usafi katika maeneo ya umma na kuimarisha afya ya Watanzania.
”Kiwango cha huduma ya maji katika maeneo ya huduma ya afya kimeimarika hivyo huduma za afya kuwa bora na salama.”amesema Dkt.Laizer
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amemuomba waziri Aweso kuweka uzito wa kutosha katika kutatua changamoto ya maji katika Jiji hilo kutokana na ongezeko la watu wanaohamia kwa kutekeleza maelekezo ya serikali.“Hatuwezi kuwa fahari ya watanzania wakati kuna baadhi ya maeneo hayana huduma ya maji na ili tuwe fahari nikuombe Mheshimiwa Aweso na najua hili unaliweza weka uzito mkubwa katika awamu hii ya tatu kwa Dodoma hii ambapo kila siku tunapokea wageni wengi ambao wanakuwa wakaazi na wanahitaji maji,”Amesema Senyamule