Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
SERIKALI Mkoani Pwani, imetoa onyo kwa wafugaji wanaotoka mikoa mingine kuacha kuingiza mifugo Yao kiholela katika maeneo hatarishi ya vyanzo vya maji Mkoani humo hali inayosababisha uchafuzi na uharibifu kwenye vyanzo hivyo.
Vilevile ,imetoa wito kwa wale wote ambao wana vibali halali vya kuendelea kutumia maji ya mto Ruvu kwaajili ya umwagiliaji wasitishe mara moja hadi hapo watakapopewa taarifa ya kuendelea kwa shughuli hizo.
Akitoa maelekezo ya mkoa ,wakati akizungumza na waandishi wa habari ,huku akiwa ameambatana na watendaji wakuu wa DAWASA pamoja na bonde la WAMI-RUVU , kuhusiana na hali ya upatikanaji wa maji na tahadhari kwa Ukosefu wa maji ,Mkuu wa mkoa wa Pwani ,alhaj Abubakari Kunenge alisema kipaombele cha kwanza ni uhai wa binadamu.
“Tunaangalia njia bora namna ya bora ya mifugo kupata maji ,Nilitoa maelekezo na kuanzisha operesheni ya kuondoa mifugo yote, changamoto yetu ni mifugo ya kuhama na kuingia katika maeneo hatarishi yenye kilimo ama vyanzo vya maji hata maeneo ambayo inaonyesha yamezidiwa wamekuwa bila mpangilio”
Pia alielekeza ,wale ambao wanaokiuka sheria na taratibu kutumia maji mto Ruvu ,kuhujumu, kufanya wizi waache mara moja .
“Sio Kama tupo katika hali mbaya Lakini Lazima tuchukue tahadhali ,vinginenyo sisi tutafanya operesheni na atakaekiuka atachukuliwa hatua,Niwaombe viongozi na wananchi kuchukua tahadhari, kuzingatia maji yaliyopo tunayatumia vizuri”alisisitiza Kunenge.
Alieleza mwaka jana Serikali ilitoa maelekezo kwamba pamoja na shughuli za kujipatia kipato, mifugo na kilimo,Wakiona kiwango cha maji kinashindwa kuwa timilivu Lazima wachukue hatua.
Kunenge aliwashukuru DAWASA kwa usimamizi mzuri wa upatikanaji wa maji safi na maji taka na ushirikiano mkubwa kutoka kwa Watendaji wa Wami-Ruvu.
Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa ,,alitoa rai kwa Wananchi Jiji la Dar es salaam na mkoa wa Pwani waanze kutumia maji kwa uangalifu.
“Maji ni Raslimali hadhimu ,tuyatunze na kuyatumia vizuri sio tunazuia wengine wasitumie maji kwa shughuli za kilimo huku wengine wakitumia maji kwa kumwagilia bustani”alieleza.
Kwa upande wa baadhi ya wakazi wa Halmashauri ya Kibaha Mjini ,na madiwani wa halmashauri hiyo walieleza tayari wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya maji kwa takariban miezi miwili sasa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji huo, Mussa Ndomba aliiomba Serikali, Mamlaka ya maji DAWASA na TANESCO kuendelea kusimamia kero hiyo ili kuondoa changamoto hiyo.
Bonde la WAMI-RUVU ambalo ni chanzo kikubwa Cha kupeleka maji Morogoro,Pwani na Pwani linaanzia milima ya Uluguru Lakini limekuwa likitumika kwa shughuli za kimaendeleo zinazohusisha maji suala ambalo linasababisha uchafuzi na kuharibu chanzo hicho, sanjali na utabiri wa Hali ya hewa kuonyesha kutokuwa na mvua za kutosha hivyo Serikali kutoa tahadhari.