Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa stendi ya mabasi na maegesho ya malori kwenye eneo la Nyamhongolo Ilemela Mwanza uliofaywa na Makamu wa Rais Mhe, Dkt Phillip Isdori Mpango.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza na Makamu wa Rais Mhe Dkt Phillip Isdori Mpango kabla ya kuzungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa stendi ya mabasi na maegesho ya malori katika eneo la Nyamhongolo Ilemela Mwanza uliofaywa na Makamu wa Rais Mhe, Dkt Phillip Isdori Mpango.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Mpango akikata utepe kuzindua stendi ya mabasi na maegesho ya malori katika eneo la Nyamhongolo Ilemela Mwanza. Kulia kwake ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe. Dkt Angeline Mabula
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe. Dkt Angeline Mabula pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Mpango wakifungua pazia kwenye jiwe la msingi la uzinduzi wa stendi ya mabasi na maegesho ya malori katika eneo la Nyamhongolo Ilemela Mwanza.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe. Dkt Angeline Mabula pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Mpango wakiangaliwe jiwe la msingi la uzinduzi wa stendi ya mabasi na maegesho ya malori kwenye eneo la Nyamhongolo Ilemela Mwanza baada ya kuzinduliwa rasmi.
Muonekano wa sehemu ya mbele ya stendi ya mabasi na maegesho ya malori kwenye eneo la Nyamhongolo Ilemela Mwanza iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Mhe. Phillip Mpango Sept 13, 2022. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
…………………………………..
Na Munir Shemweta, MWANZA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula amemshukuru Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha wizara yake kupata fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 50 kwa ajili ya programu ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi nchini.
Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iliipatia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 50 kwa ajili ya kuzikopesha Halmashauri 55 kutekeleza Programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi nchini.
Alisema, utolewaji wa kiasi hicho cha fedha kumewezesha mkoa wa Mwanza kupatiwa shilingi Bilioni 6.691 zilizosaidia kutekeleza miradi ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Dkt Mabula ametoa shukran hizo tarehe 13 Septemba 2022 jijini Mwanza mbele ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt Phillip Isdori Mpango wakati wa uzinduzi wa stendi mpya na ya kisasa ya mabasi na maegesho ya malori iliyopo eneo la Nyamhongolo wilayani Ilemela.
Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, uwezeshwaji wa pesa uliofanywa na serikali katika sekta ya ardhi umeisadia halmashauri yake ya manispaa ya Ilemela kuwa na mradi wa kuuza viwanja alioueleza kuwa umeonesha mafanikio makubwa.
“Kuhusu masuala ya ardhi, ninamshukuru Rais wetu mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Wizara shilingi bilioni 50 na kati ya kiasi hicho mkoa wetu wa Mwanza umepata bilioni 6.91 pesa ambazo zimeisadia sana zoezi la upimaji viwanja katika halmashauri zetu ikiwemo halmashauri ya manispaa ya Ilemelaa” alisema Dkt Mabula.
Hata hivyo, Dkt Mabula ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ilemela mkoani Mwanza alisema, mbali na mhe Rais kuisadia sekta ya ardhi lakini kuna juhudi kubwa zimefanywa na serikali ya awamu ya sita katika mkoa wa Mwanza hususan kwenye masuala ya miundombinu, uchukuzi pamoja na huduma za afya jambo alilolielezea kuwa, limejenga imani kwa wananchi.