Adeladius Makwega-MAKOLE
Niliwasiliana na ndugu yangu mmoja katika simu yake ya mkononi nikimuuliza ushiriki wa vyama vya wafanyakazi katika menejimenti na bodi za mashirika ya umma ukoje?
Ndugu yangu huyu alinjibu kwa maneno haya,
“Kwa sasa vyama vya wafanyakazini vingi ni vibogoyo na ukitumia nguvu sana wanakuumiza, kuna wakati wenzetu walitafautiana sana na mkuu wa shirika letu, wakaondolewa kushiriki katika vikao wa menejimenti. Mkuu wa taasisi hii akasema sioni sababu ya kuwaalika katika menejimenti yangu, akawatoa, ulipochaguliwa uongozi mpya ukaukaribisha katika menjimenti hiyo lakini kulikuwa na mkurugenzi mmoja wa utawala akasema sheria haisemi kuwa viongozi wa wafanyakazi waingie katika menejimenti au bodi kwani wao siyo sehemu ya menejimenti, tukawa hatushiriki menejimenti wala kikao chochote kile.”
Viongozi wa wafanyakazi wakiwa na jambo basi wanaweza kuwafuata utawala na kuongea nao au wanaweza kulisema katika vikao vya watumsihi wote, hakuna vikao rasmi viongozi hao wanashirikishwa labada katika baraza la wafanyakazi tu.
Ndugu huyu aliniambia kuwa wakati wa ujamaa kikaoa cha uongozi wa shirika na wafanyakzi wote kinafunguliwa na mwenyekiti wa wafanyakazi, vikao wa menejimenti hadi bodi wafanyakazi wakiwa na mwakilishi wao. Kwa sasa mambo yanapangwa na viongozi , menejimenti hadi bodi ukija katika utekelezaji yanakwama na hata ukija wakati wa Baraza la Wafanyakazi mambo yameshaharibika.
Kwa kuwa ndugu huyu aliwahi kuwa kiongozi wa Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania nilimuuliza je hii bodi mpya unaionaje?
“Hii ni bodi ya kawaida sana, tunafahamiana basi tunakumbukana, jamani mnikumbuke miniweke katika bodi fulani, haina msaada, wapo Watanzania wenye mawazo mazuri wanafariki nayo, wapo wanaolifahamu shirika hilo, wapo wanaoweza kukamilisha mipango mizuri ya shirika hilo, lakini hawapewi.”
Ndugu yangu huyu akaniongeza neno kwa kusema kuwa, kwa hali ya sasa cha kufanya, ni kujipanga na kwenda sawa nao ili maisha yasonge tu, mfumo wa kiutendaji wakuonesha umahiri na uhodari haupo, “Ukifika sehemu ukitaka kufanye mabadiliko yaonekane utakuwa unaongelea huko mwenyewe, watakupiga majungu na kukukandamiza tu “
Haya ni maneno mazito sana kutoka kwa ndugu yangu huyu lakini ndiyo ukweli wa mambo aliyazungumza kutoka moyoni kwa jambo ambalo analifahamu, huku akimsimulia nduguye.
Alipokata simu ndugu huyu nilikumbuka kuwa, Agosti 23, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alifanya uteuzi wa ndugu Stephen Kagaigai kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (SHIUTA) akichukua nafasi ya Balozi Herbert Mrango ambaye alimaliza kipindi chake. Majuma mawili baadaye waziri mwenye dhamana na habari alifanya uteuzi wa wajumbe wa bodi ya shirika hilo akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Tuma Abdallah, mtangazaji wa zamani wa shirika hilo na mbunge wa zamani, Amina Mollel, mkuu wa kitengo cha mawasilianoa serikalini wa Wizara ya Habari na Tekinolojia ya Habari Innocent Mungy, Cosmas Mwaisobwa, Mwanjaa Lyezia, Dr Hidelbrand Shayo na Justina Mashiba.
Huku bodi hii ya Shirika la Utangazaji Tanzania ikiwa ni ya tatu tangu kuanzishwa kwa shirika hilo, ikitanguliwa na bodi ya Profesa Mwajabu Possi, Balozi Injini Herbati Mrango na ya sasa ya Ndugu Stephen Kagaigai na shirika hili likiongozwa kwanza na Dastan Tido Mhando, Clement Mshana na huyu wa sasa.
Swali la kujiuliza je Bodi ya Stephen Kagaigai inaweza kuleta mabadiliko ya utayarishaji wa vipindi bora, taarifa bora, kurudisha imani ya Watanzania katika chombo hiki kilichokuwa kikiaminiwa sana wakati wa uhuru, baada ya uhuru na wakati wa ujamaa uliombatana na harakati za ukombozi wa bara la Afrika ?
Kama kweli RTD ilifanya kazi kwa uhodari katika vipindi hivyo ikiwamo harakati za ukombozi wa bara la Afrika? Je Shirika la Utangazaji Tanzania sasa linashindwa nini kuweka mikakati na kuirejea kileleni katika ukombozi wa sasa wa fikra(kuaminiwa), ukombozi wa kilimo, ukombozi wa ufugaji, ukombozi wa elimu, ukombozi biashara, ukombozi wa ujasiriamali ? Na hata ukombozi wa afya na tiba? Kwa kufanya hivyo ni kuwaakomboa Watanzania .
Swali la kujiuliza au zile chembechembe za harakati za ukombozi waliondoka nazo wazee walioshirikiana na viongozi wa wakati huo za wapigania uhuru? Au sasa ni wakati sahihi wa kulivunja shirika hilo na kuunda chombo kingine kitakachoaminiwa?
Nihitimishe tu kwa kusema kuwa Waziri Habari Nape Nnauye ndiye aliyewateua wajumbe wa Bodi ya Balozi Mrango, wengi wanaitazama bodi hii ya Balozi Mrango haikufanya vizuri. Sasa Waziri wetu yule yule ameteua bodi ya taasisi ile ile inayoongozwa na ndugu Kagaigai .
Bodi ya Profesa Mwajabu Possi haikufanya vizuri lakini ilibebwa tu na utendaji kazi wa wa kujituma wa Dastani Mhando. Hata Mhando alipoondoka tu bodi hiyo ilipwaya, ikiaminika kuwa Dastani Mhando aliondoka na imani aliyoijenga kwa wasikilizaji na watazamaji wa TBC kwa muda aliokuwepo hapo.
Binafsi sina mashaka ya watu wanne katika bodi hii Mwenyekiti Stephen Kagaigai, Amina Mollel, Tuma Abdallah na Innocent Mungi. Nikuume sikio msomaji wangu, TBC inamiliki maeneo makubwa ya ardhi nchi nzima na yapo katika maeneo muhimu kama yangetumika kibiashara yangesaidia TBC na nchi yetu pia mathalani eneo la Ubungo External, ardhi hizo kwa sasa zinamilikishwa taasisi zingine, Je TBC yenyewe inao mpango wowote wakuitumia ardhi hiyo kiuwekezaji ?