Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Saad Mtambule akimkabidhi kombe bingwa wa Mashindano Sao Hill Misitu auto Cross Tanzania The Royal Tour
Moja ya magari ambayo yalishiriki katika Mashindano Sao Hill Misitu auto Cross Tanzania The Royal Tour
Moja ya magari ambayo yalishiriki katika Mashindano Sao Hill Misitu auto Cross Tanzania The Royal Tour
Hizi na zawadi ambao washindi wa Moja ya magari ambayo yalishiriki katika Mashindano Sao Hill Misitu auto Cross Tanzania The Royal Tour walipewa
Na
Fredy Mgunda,Iringa.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Dk Pindi Chana amevutiwa na ubunifu na
mawazo mazuri yaliofanywa na Shamba la Serikali Sao hili kwa kuandaa
Mashindano ya mbio za Magari katika msitu huo kwani ni fursa kubwa ya kutangaza
vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo kwenye Shamba hilo.
Balozi
Dk Chana ameyasema Hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu katika Mashindano
Sao Hill Misitu auto Cross Tanzania the Royal Tour kwa kushirikiana Iringa
Motorsports club Tanzania kwa ubunifu huo kwani unaumuhimu mkubwa katika
masuala mazima ya kutangaza utalii.
”
Haya nimaelekezo ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan ambaye alituelekeza kuendelea
kubuni vyanzo mbalimbali vya utalii kwani ndio chanzo kimoja wapi katika
masuala mazima ya utalii wa aina hiyo wa mashindano ya mbio za mahari au Rally
katika misitu yetu ambavyo tunaihifadhi mwenye maeneo yetu .” Alisema
dk Balozi Chana
Aidha
alieleza Mkakati wa wizara ni kunatukio masuala ya michezo mbalimbali
ambayo utafanyika katika maeneo ya hifadhi za Serikali ikiwemo msitu
katika eneo la Sao hill.
”
Ni jambo zuri na tuendelee kuratibu ili liweze kufanyika mara kwa mara
kadiri Kamati ya maandalizi tutakavyo amua I’ll kupata washiriki wengi
zaidi.” Alisema Waziri huyo
Kwa
upande wake Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Sao hill Lucas Sabida alisema wameandaa
mashindano mafupi ya mbio za mahari lakini wanampango wa kuandaa mashindano
makubwa zaidi.
Alisema
lengo la mashindano Hayo ni kuendelea kujitangaza kama Shamba la TFS kwa
ajili kutangaza utalii wa ikolojia na nyuki kupitia utalii wa michezo wa
mbio za Magari kutokana na mwitikio kuwa mkubwa kwao Wananchi.
Mkuu
wa Wilaya ya Mufindi Saad Mtambule alisema kuwa wilaya hiyo inamisitu Msingi
ambapo wanaziadi ya hekta 100,000 ambayo inatumiwa kwa ajili ya uzalishaji wa
mbao pamoja na bidhaa zingine kama Marine boad, Mirunda na nguzo za
umeme.
Alisema
mazao Hayo wamekuwa wakiyatumia na kuwasaidia kwa uchumi na mapato kwa
mustakabali wa jamii lakini kupitia Program ambayo ilianzishwa na Rais wa
Jamhuria ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan The Royal Tour.