Mwenyekiti Msaidizi wa Taasisi ya Wanawake laki moja, Bi.Nangasu Warema akizungumza na waandishi wa habari jana Septemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea Kongamano la Wanawake na Utalii linalotarajia kufanyika Oktoba 15,2022 Serena Hoteli Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti Msaidizi wa Taasisi ya Wanawake laki moja, Bi.Nangasu Warema akizungumza na waandishi wa habari jana Septemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea Kongamano la Wanawake na Utalii linalotarajia kufanyika Oktoba 15,2022 Serena Hoteli Jijini Dar es Salaam.
akizungumza na waandishi wa habari jana Septemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea Kongamano la Wanawake na Utalii linalotarajia kufanyika Oktoba 15,2022 Serena Hoteli Jijini Dar es Salaam.
****************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
TAASISI ya Wanawake Laki moja wameandaa kongamano kubwa la Wanawake na Utalii kwaajili ya kuhamasisha wanawake kuhusu fursa zilizopo kwenye sekta ya Utalii ambapo kwa asilimia kubwa waliopo kwenye sekta ya Utalii ni wanawake.
Akizungumza na waandishi wa habari Jana Septemba 12,2022, Mwenyekiti Msaidizi wa Taasisi ya Wanawake laki moja, Bi. Nangasu Warema amesema kongamano hilo litafanyika Oktoba 15,2022 katika ukumbi wa Serena Hoteli Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa Utalii.
“Tumeona hivi karibuni utalii umekuwa sana na Idalii ya takwimu ya Serikali imetueleza kwamba Utalii umekuwa kuanzia mwezi January mpaka julai kwa 62.7%. Sisi tumekuja kuwaeleza wanawake mbalimbali fursa zilizopo kwenye Sekta ya Utalii”. Amesema Bi.Warema.
Amesema Utalii ni Sekta mtambuka ambayo imebeba mambo mbalimbali Kama watu wa Afya, Marubani, Mama Ntilie, Wasafirishaji wote kwa pamoja wanaguswa na Sekta ya Utalii.
Nae Mshauri wa Utalii na Uchumi katika Taasisi ya Wanawake laki moja Bi.Theresa Mgobi amesema Siku hiyo kutauwa na Mafunzo ambayo Mwanamke yataweza kumsaidia kiuchumi kutokana na utalii na kuepukana na Umasikini.
Aidha amesema fursa zilizopo kwenye sekta ya Utalii ni pamoja na Tehema na Utalii, ambapo watalii wanaokuja Tanzania wanapata taarifa kwa kutumia simu/ Mtandao akishafika anatumia mtandao kufika aendako ikiwa 3.1% tu ya Watalii wanaofaidika na mtandao Tanzania.
Amesema fursa nyingine ni pamoja na Utalii wa kitamaduni ambapo Tanzania kuna Makabila mbalimbali ambayo wanaweza anzisha Utalii wa Kitamaduni. Mabenki wanaweza kusaidia katika kusaidia wakina Mama wenye maono ya Utalii.