Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt.Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuingia makubaliano ya ushirikiano na Serikali ya China katika Sekta ya Takwimu. Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Zanzibar Bw.Mohammed Ali Hamza akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuingia makubaliano ya ushirikiano na Serikali ya China katika Sekta ya Takwimu. Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuingia makubaliano ya ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika Sekta ya Takwimu.
*********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SERIKALI ya China na Tanzania zimeingia makubaliano kushirikiana kwenye sekta ya Takwimu ambapo China imeipongeza Tanzania kwa kufanikisha zoezi la Sensa ya watu na Makazi ambayo ilifanyika kuanzia Agosti 23,2022.
Akizungumza leo Septemba 12,2022 Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt.Albina Chuwa amesema ushirikiano huo kati ya Tanzania na China utaimarisha kwa kiasi kikubwa sekta hiyo.
“Kupitia mpango wa kitaifa wa kuimarisha na kuboresha takwimu tulimaliza awamu ya kwanza, katika awamu ya pili ndipo tutakapoanzia kwenye ushirikiano huu,” amesema Dkt.Chuwa.
Amesema miongoni mwa mahitaji ambayo Serikali ya Tanzania imeyawasilisha ni kuimarishwa kwa uwezo na miundombinu ya Takwimu.
Nae Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian amesema dhamira ya ushirikiano huo ni kuboresha upatikanaji wa takwimu ikiwa China tulifanya sensa mwaka 2022 ambalo ni jambo la muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Zanzibar Bw.Mohammed Ali Hamza ameeleza kuwa makubaliano hayo yatasaidia kuendelea kushirikiana katika hatua iliyofikiwa sasa ikiwemo uchambuzi wa data.