***********************
Na. Abel Paul wa Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limesema kuwa tarehe 10.09.2022 muda wa 02:00 usiku huko Kijiji cha Endabashi tarafa ya Endabashi Wilaya ya Karatu Mkoa wa Arusha Jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata mmtu mmoja REGINALD AMBROS maalurufu Amsi (42) mkulima mkazi wa Endabashi akiwa na vipande viwili vya Jino la Tembo ambavyo alikuwa amevifunga ndani ya boksi.
Akitoa taarifa hiyo leo tarehe 12 agosti kamanda wa Poloisi mkoa wa kamishina msaidizi wa Polisi ACP JUSTINE MASEJO amesema kuwa Jeshi hilo liliendesha operesheni maalum katika wilaya ya karatu na kufanikiwa kukamata mtuhumiwa kutokana na taarifa za wananchi wenye mapenzi mema na rasilimali za nchi ambazo zimekuwa zikiliingizia Pato taifa ikiwa ni Pamoja na fedha za kigeni.
Ambapo amebainisha kuwa uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akijihusisha na matukio ya biashara haramu ya uuzaji wa nyara za serikali ambapo Jeshi la Polisi linaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo ilikupata mtandao mzima.
Kamanda Masejo alieleza kuwa Jeshi hilo lilifanikiwa kukamata jumla ya lita 1480 za pombe haramu aina ya gongo, mitambo 80 ya kutengeneza Pombe hiyo Pamoja na watuhumiwa 62 ambao wamefikishwa mhakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
JELA MIAKA 80 KWA KOSA LA UBAKAJI
Katika hatua nyingine Kamanda masejo amewaambia waaandishi wa habari kuwa katika kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia katika mkoa wa Arusha Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwa kamata watuhumuwa wawili ambao ni PAUL HILONGA (60) mkazi wa Karatu kwa kosa la kubaka mwingine ni ERASTO SIAS 24 mkazi wa Qurus wilaya ya karatu kwa kosa lakubaka mtoto mwenye umri wa miaka 08 amabapo kwa pamoja wote wamefungwa miaka 80 uku akibainisha kuwa mshitakiwa Paul Hilonga amefungwa kifungo cha miaka 50 jela na Erasto Sias amefungwa 30 jela.
katika hatua nyingine Kamanda Masejo amekutana na askari katika wilaya ya Karatu na kubainisha kuwa lazima tukubali ukweli kuwa kuna baadhi yetu wanaenda kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi ambapo amewaambia askari kuwa hato sita kuchukua hatua kwa askari wasio zigatia nidhamu haki welledi na udalifu kwa atakaye Kwenda kinyume na mwendo mwema wa Jeshi la Polisi.