Afisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Msaidizi Damian Muheya, akitoa maelezo ya huduma zitonazotolewa kwenye banda la Jeshi hilo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mstaafu Methew Mwaimu, alipotembelea banda la Jeshi hilo mapema leo tarehe 11 Septemba, 2022.
Sajini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Immaculata Liyombo, akitoa maelezo ya ukaguzi wa kinga na tahadhari ya majanga ya moto kwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Nchini, Jiji Mstaafu Mheshimiwa Methew Mwaimu, wakati alipotembelea banda la Jeshi hilo leo tarehe 11 Septemba, 2022. (Picha zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
***********************
DODOMA, SEPTEMBA 11, 2022
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linashiriki katika Maadhimisho ya Miaka 20 Tangu Kuanzishwa kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jijini Dodoma katika Viwanja vya Jakaya Kikwete “Conversion Center”, maonesho hayo yaliyoanza Septemba 10, 2022 yatakayofungwa Septemba, 15 2022 yameshirikisha Taasisi za Umma, Binafsi pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatumia maonesho hayo kama jukwaa la kutoa elimu ya kinga na taadhari dhidi ya majanga mbalimbali sanjari na kuufahamisha umma majukumu mengine ya Jeshi hilo.
Kupitia maonesho hayo Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binandamu na Utawala Bora, Jaji Mstafu Mheshimiwa Methew Mwaimu, ametembelea banda la Jeshi hilo mapema leo Septemba 11, 2022 na kupata elimu hiyo.
Mheshimiwa Methew, alielezwa huduma zinazopatikana kwenye banda hilo ni elimu kwa umma juu ya kinga na tahadhari dhidi ya moto, ukaguzi na umuhimu wake kwenye majengo na vyombo vya usafiri, umuhimu wa kupitisha michoro ya ramani za majengo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, haki ya huduma zinazotolewa na Jeshi hilo pamoja na utumiaji wa vifaa vya kuzimia moto pamoja na majukumu ya Jeshi hilo kwa ujumla.
Aidha Wananchi mbalimbali wametembelea banda hilo na kupata elimu ikiwa ni pamoja na kutoa maoni na kuuliza maswali mbalimbali na kupatiwa majibu, ambao kati yao wamefurahia uwepo wa Jeshi hilo kwenye maadhimisho hayo.
Naye Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Damian Muheya, amewaomba Wananchi wa Jiji la Dodoma kutembelea maadhimisho hayo ili wapate elimu mbalimbali kutoka kwenye mabanda mbalimbali likiwemo na Banda la Jeshi hilo.