
Kamishina wa Ardhi Mkoa wa Mwanza Elia Kamihanda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)juu ya uzinduzi wa kituo jumuhishi cha kutolea Hati za viwanja kilicho zinduliwa leo Septemba 9,2022

Mkuu wa idara ya Mipangomiji na Ardhi Manispaa ya Ilemela Shukrani Kyando,akizungumza namna ambavyo Serikali imeikopesha Halmashauri hiyo fedha kwaajili ya mradi wa viwanja

Baadhi ya Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waliojitokeza kwaajili ya kukamilisha taratibu za kupata Hati

Yusuphu Manyonyi akipokea Hati Miliki ya kiwanja kutoka kwa Kamishina wa Ardhi Mkoa wa Mwanza Elia Kamihanda.

Safia Mkama akipokea Hati kutoka kwa Kamishina wa Ardhi Mkoa wa Mwanza Elia Kamihanda
………………………..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Ofisi ya aridhi Mkoa wa Mwanza inamalengo ya kutoa hati elfu 50 za viwanja kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Septemba 9,2022 kwenye uzinduzi wa kituo jumuhishi cha kutolea hati kwenye viwanja vya Rock City Mall katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Kamishina wa Ardhi Mkoani hapa Elia Kamihanda, amesema lengo la kutoa hati hizo ni kuhakikisha kazi zote za urasimishaji wa makazi zinakamilika kwa wakati ifikapo mwaka 2023.
Amesema wameanza kutekeleza maelekezo ya Wizara ya Ardhi ya kuwepo kwa vituo jumuhishi vitakavyosaidia utoaji wa hati kwa haraka na hadi sasa kwenye kituo walichokizindua leo Wananchi 55 wamekamilisha taratibu za upatikanaji wa hati na wamepewa hati zao.
Amesema zoezi hilo la vituo jumuhishi litasaidia kuondoa malalamiko kwa Wananchi ya ucheleweshwaji wa upatikanaji wa hati.
Katika hatua nyingine Kamihanda amesema kuwa wamezindua programu ya uuzaji wa viwanja vya Manispaa ya Ilemela ambavyo vimepimwa kwenye utaratibu wa miradi ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi.
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Mipango miji na Ardhi kutoka katika Manispaa ya Ilemela Shukrani Kyando, amesema Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeikopesha Halmashauri hiyo sh. Bilioni 3.6 kwaajili ya mradi wa viwanja ambavyo vimeanza kuuzwa.
Yusuphu Manyonyi na Safia Mkama ni miongoni mwa Wananchi waliojitokeza kwenye zoezi la uzinduzi wa kituo jumuhishi cha kutolea hati ambapo wamesema utaratibu huo ni mzuri kwani utasaidia kuondoa ucheleweshaji wa upatikanaji wa hati kwa wananchi ambao ulikuwepo awali.