Furaha ikitawala wakati wa hafla hiyo. |
Na Dotto Mwaibale, Singida
SHIRIKA la Elizabeth Glaser Pediatic Aids Foundation (EGPAF) kupitia Mradi
wa USAID Afya Yangu Northern limetoa
magari mawili Mkoa wa Singida yenye thamani ya zaidi ya Milioni 91.9 kwa ajili
ya kusaidia usimamizi na ufuatiliaji wa huduma za afya mkoani hapa.
Akizungumza wakati wa hafla ya
kukabidhi magari hayo Mkurugenzi Mkazi wa Shirika hilo, Dk. Sajida Kimambo
alisema magari hayo yatazisaidia timu za
usimamizi wa huduma za afya ngazi ya mkoa na wilaya hivyo yatachagiza kasi na
ufanisi wa utoaji wa huduma bora kwa wananchi .
Alitaja gari hizo kuwa ni Toyota Land Cruiser DFP 6673 yenye thamani ya
kiasi cha Sh.42,250,334/= itakayo kwenda kwa timu ya usimamizi wa afya ngazi ya
mkoa (RHMT) na gari aina ya Nisssan Pick Up DFP
9272 yenye thamani ya kiasi cha Sh. 49,433,008 kwa ajili ya timu ya usimamzi wa
afya halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na
kuwabei ya manunuzi ya magari hayo ni za mwaka 2010.
Akizungumzia utendaji kazi wa shirika hilo katika kipindi cha robo mwaka tatu
za utekelezaji wa Mradi wa USAID Afya Yangu Northern Dk.Kimambo
alisema mradi huo Kanda ya Kati na Kaskazini, ulianza Mwezi Novemba mwaka wa Jana,
(2021) na unajikita katika afua za mapambano ya UKIMWI/VVU, Kifua Kikuu Lakini
pia uzazi wa mpango, na mapambano dhidi ya UVIKO-19.
“Mradi huu umekua ukifanya kazi kwa mashirikiano makubwa na serikali
kupitia wizara za afya na TAMISEMI, pamoja na timu za usimamizi wa huduma za
afya ngazi ya mkoa na wilaya, katika mikoa sita ya Arusha, Dodoma ,
Kilimanjaro, Manyara, Tabora na hapa Singida na kuwa upo katika wilaya 44 na
vituo 588 na kwa Mkoa wa Singida upo katika halmashauri zote saba na vituo themanini
na tisa” alisema Dk.Kimambo.
Alisema mradi huo umepanga shughuli za afya katika Mkoa wa Singida kwa
mwaka wa fedha 2022/2023 zenye Jumla ya Sh. Millioni mia saba ishirini na tano,
laki nne, sitini na nane elfu mia nne na sitini. (725,468,460 TZS) na kuwa pesa
hizo zote zitakwenda moja kwa moja katika halmashauri na tayari zimekwisha anza
kutolewa katika halmashauri hizo ,RHMT na Hospitali ya Mkoa kwa awamu.
Kimambo alisema mradi huo pia umepanga kutoa zaidi ya million mia nne kwa
mwaka wa fedha 2022/2023 kutoka makoa makuu ya Taasis hiyo , hivyo kufanya
thamani ya jumla ya bilioni moja za kitanzania kutoka katika shirika hilo
kwenda Mkoa wa Singida kwa mwaka
2022/2023.
Aidha Kimambo alisema kuwa mradi huo
umetoa vifaa nane vya matibabu ya viashiria vya saratani ya shingo ya kizazi
viitavyo thermos coagulation machine vyenye thamani ya Sh.Mmillion mia moja
ishirini (120,000,000/=TZS), ambavyo vipo vituoni tayari vikiendelea kutoa
huduma kwa wananchi.
Alisema mradi huo pia umeweka mifumo ya TEHAMA katika vituo vya afya kwa
ajili ya kutunza kumbukumbu (data management systems) ambapo kompyuta mpakato 21
na zile za mezani 34 zilinunuliwa na kufungwa katika vituo vya afya 40 zenye
thamani ya zaidi Sh.116.7
Pia alisema mradi huo una saidia
usafirshaji wa sampuli za binaadamu kutoka vituo vyote mkoani kupitia mkataba
na shirika la Posta na kampuni ya TUTUME, kwa kila Mwezi kulipia wastani wa
kiasi cha shillingi million ishirini na tano na kuwa unalipia gharama za vipimo
vya wahisiwa wa kifua kikuu wanaopaswa kupatiwa vipimo vya mionyo, lakini
vipimo cha biochemistry kwa wateja wakifua kikuu sugu na wateja wa dawa kinga
za VVU.
Alisema katika kutambua changamoto za akidi isiyo timilifu ya watumishi wa
afya katika vituo vya kutolea huduma za afya, mradi wa USAID Afya Yangu kwa
kushirikiana na Afya endelevu umeajiri watumishi wa kanda mbali mbali za afya
wapatao sabini na moja (71) katika vituo mbali mbali vya afya mkoani Singida na kuwa pia unawezesha watoa
huduma ngazi ya jamii wapatao mia mbili sabini katika vituo mbali mbali ili
kuchagiza utoaji wa huduma za afya katika jamii.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akipokea magari hayo alisema
yaende yakatumike kwa kazi iliyokusudiwa na kuwa atakuwa mkali katika
kuyasimamia na watu watamuona mbaya katika usimamizi wake.
Mkururgenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Melkzedeki Humbe alilishukuru shirika hilo
kwa msaada huo na kuwa gari walilopewa litafanya kazi kwa ajili ya timu ya
usimamizi wa afya katika halmashauri hiyo na si vinginevyo.