Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania – TCRA imeelezea kujidhatiti katika kusimamia ukaguzi wa taka za kielektroniki, kwalengo la kuhakikisha Ukaguzi wa vifaa hivyo unafanyika kabla ya vifaa hivyo havijaingia nchini, ili kulinda mazingira dhidi ya taka za kielektroniki hasa vifaa vya kielektroniki vinapofikia ukomo wa matumizi.
Akizungumza jijini Dar es salaam jana, Meneja wa Usimamizi wa Mawasiliano na Intaneti wa TCRA Mhandisi Saddath Kalolo amesisitiza kuwa Mamlaka hiyo katika kuratibu usimamizi wa taka za kiektronikia kama ilivyoainishwa kwenye sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 kupitia maboresho ya yaliyofanyika mwaka 2019, TCRA inao wajibu wa kuratibu usimamizi vifaa vya kielektroniki vinapofikia mwisho wa matumizi.
“Ili kufanikisha utekelezaji wenye tija katika usimamizi wa taka za kielektroniki TCRA tunashirikiana na wadau mbalimbali wa mazingira wakiwemo Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (WHMTH), Baraza la Taifa la Mazingira-NEMC, Tume ya TEHAMA na wadau binafsi wanaohusika na kukusanya taka za kielektroniki, miongoni mwa wengine,” alisisitiza Kalolo.
Kutokana na Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Viwango vya Vifaa na Usimamizi wa Taka za Kielektroniki), 2020 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inalo jukumu la kuratibu usimamizi wa taka za kielektroniki; hii ni kutokana na kwamba uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na taka za kielektreoniki umekuwa ukiongozeka kwa kazi kila uchao na kusababisha athari katika mazingira.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mwaka 2017 inaonyesha taka za kielektroniki zinaongezeka kwa kasi kubwa, hasa katika nchi zinazoendelea. PICHA: MTANDAO
“Kanuni za Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta (Viwango vya vifaa vya kielekroniki na usimamizi wa taka za kieletroniki) za mwaka 2020 zimeleekeza majukumu ya wadau mbalimbali wakiwemo wanaoingiza vifaa vya kielekroniki nchini pamoja na kuweka utaratibu wa kukusanya taka za kielektroniki ili kuwezesha usimamizi makini wa taka za kielekroniki, TCRA tumejidhatiti kusimamia utekelezaji wa jukumu hili la kikanuni,” alisisitiza Kalolo.
Itakumbukwa kwamba uchafuzi wa mazingira utokanao na utupaji hovyo wa taka za kielektroniki umesababisha Umoja wa Mataifa kuweka msisitizo wa udhibiti wa utupaji wa taka hizo, ambapo Kalolo alisisitiza kwamba TCRA inatekeleza jukumu la kudhibiti taka za kielektroniki kwa kuzingatia miongozo ya Umoja huo kupitia Shirika la Kimataifa la Mawasiliano-ITU. TCRA imetoa wito kwa wadau mbalimbali wa mazingira na wananchi kwa ujumla katika kufanikisha utunzaji wa mazingira unaotokana na utupaji sahihi wa taka za kielktroniki.