MENEJA wa mradi wa Pamoja Tuwekeze Afya (PATA),Dk Godfrey Kway,akielezea jinsi mradi huo unavyoendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya kwenye makanisa wakati wa mkutano wa 85 wa Chama cha Madaktari wa Hospitali za Mashirika ya Dini(TCMA) unaoendelea jijini Dodoma.
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kikristu (TCMA) Dk.Paul Kisanga,akifafanua mada mbalimbali zilizowasilishwa kwenye mkutano wa 85 wa Chama cha Madaktari wa Hospitali za Mashirika ya Dini(TCMA) unaoendelea jijini Dodoma unaoendelea jijini Dodoma.
Dk Ringo Mtei kutoka Shirika la Christian Social Services Commission (CSSC),akitoa mada kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa 85 wa Chama cha Madaktari wa Hospitali za Mashirika ya Dini (TCMA) unaoendelea jijini Dodoma.
Mganga Mfawidhi kutoka Hospitali Teule ya St.Joseph Moshi Sister Dk Hellen Kyilosudu,akielezea namna ya kuendesha hospitali kwa faida na kupitia mafunzo ya Shirika la Christian Social Services Commission (CSSC), kupitia mradi wa Pamoja Tuwekeze Afya wakati wa mkutano wa 85 wa Chama cha Madaktari wa Hospitali za Mashirika ya Dini(TCMA) unaoendelea jijini Dodoma.
MGANGA Mfawidhi kutoka Hospitali ya Turiani Morogoro,akiwasilisha mada kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa 85 wa Chama cha Madaktari wa Hospitali za Mashirika ya Dini(TCMA) unaoendelea jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano wa 85 wa Chama cha Madaktari wa Hospitali za Mashirika ya Dini(TCMA) unaoendelea jijini Dodoma.
MWENYEKITI Chama cha Vituo Binafsi vya Afya Tanzania (APHFTA) Dk.Egina Makwabe,akichangia mada wakati wa mkutano wa 85 wa Chama cha Madaktari wa Hospitali za Mashirika ya Dini(TCMA) unaoendelea jijini Dodoma.
MGANGA Mfawidhi Hospitali ya Kilema Sr.Dk.Mayola Massawe,akitoa ushauri kwa washiriki wakati wa mkutano wa 85 wa Chama cha Madaktari wa Hospitali za Mashirika ya Dini (TCMA) unaoendelea jijini Dodoma.
……………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
SHIRIKA la Christian Social Services Commission (CSSC), kupitia mradi wa Pamoja Tuwekeze Afya unaolenga kuwezesha vituo vya afya vya makanisa kujiimarisha na kujiendesha kiuendelevu kupitia mapato ya ndani umeleta mafanikio mbalimbali ikiwemo kuongeza wateja kwa asilimia 22 pamoja na kuongeza mapato ya hospitali kwa wastani wa asilimia 34 kwa mwezi.
Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Meneja wa mradi huo,Dk Godfrey Kway wakati akizungumza kwenye mkutano wa 85 wa Chama cha Madaktari wa Hospitali za Mashirika ya Dini(TCMA)
Dk Kway amesema kuwa mradi huo unalenga kuimarisha vituo vya makanisa ili viweze kujitegemea kifedha.
Amesema kupitia mradi huo vituo vya afya 11 vimeweza kufikiwa hadi sasa na vinatoa huduma bora kwa wananchi katika maeneo ya vijijini.
“Vituo vyetu vimekua vikitegemea ufadhili na fedha kutoka nje. Sasa hivi ufadhili umepungua na vimeanza kupata changamoto kutokana na fedha hizo kupungua.
“Tuliona kama kanisa tuje na mradi huu ili kuvisaidia vituo hivi kuongeza ubora na mapato na kutengeneza huduma zao pamoja na kuboresha huduma za uongozi ili kuwavutia wagonjwa na pamoja na kutatua changamoto ya kukosekana kwa dawa
“Mpaka sasa tumeanza kupata mafanikio makubwa cha kwanza ilikuwa kutoa uelewa kwa viongozi wetu wa dini.Vituo vimeanza kupata mafanikio makubwa hasa kwenye bima kwani mapato ya mwezi yameongezeka maradufu ndani ya mwaka,” amesema Dk Kway.
Kwa upande wake,Dk Ringo Mtei kutoka Shirika la Christian Social Services Commission (CSSC), amesema jukumu lao kubwa ni kuhakikisha vituo hivyo vya afya vya kanisa vinatoa huduma bora kwa wananchi na kuweza kukamilisha lengo la kutoa huduma kwa watu wasiojiweza.
“Tunatekeleza mradi wa Pamoja Tuwekeze Afya ambao unalenga vituo vya kanisa kutoa huduma bora kujitegemea na kuendelea kutoa huduma endelevu.
“Tumefanya kwa kuanzisha na kuimarisha kampuni ya madawa ambayo itakuwa inasambaza madawa. Vilevile kuwezesha vituo hivi kutumia njia mbadala za kuweza kupata mikopo, pamoja na kuboresha miundombinu kwani mingi ni ya zamani kutokana na vituo vingi vimeanzishwa zaidi ya miaka 100,” amesema.
Amesema lengo ni vituo viweze kujiendesha kutokana na vitengo vyao vya ndani na kuvisaidia kupata mikopo ambayo itawasaidia kujitegemea na kutoa huduma endelevu na zenye ubora.
“Changamoto ilikuwa ni vituo haviwezi kujiendesha vingine hata kulipa mishahara ilikuwa ni shida na hata dawa zilikuwa hazipatikani na vituo tulikuwa tukiwategemea wahisani,”amesema.
Naye,Mganga Mfawidhi kutoka Hospitali Teule ya St.Joseph Moshi Sister Dk Hellen Kyilosudu, amesema wamepata mafunzo mbalimbali ya namna ya kuendesha hospitali kwa faida na kupitia mafunzo hayo mafaniko makubwa yameonekana.
Amesema wanahakikisha wanatoa huduma bora kwa wagonjwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanaondokana na uhaba wa dawa, wafanyakazi wote kufuata miongozo na kujiwekea malengo na kutunza kumbukumbu zao vizuri ili kuepukana na upotevu wa mapato unaotokea katika maeneo mbalimbali.
“Tulikua na udhaifu kwenye makusanyo ya mapato hasa kwa upande wa bima za afya, baada ya kupata mafunzo na usaidizi wa mradi wa Pamoja Tuwekeze Afya sasa tumeweza kuboresha huduma zetu na wananchi wanakuja kwenye kituo chetu na sasa mapato yameongezeka.” amesema.
Mradi wa Pamoja Tuwekeze Afya unatumia mkakati wa kufanya mapitio ya masoko ya vituo vya afya vya makanisa ikiwemo aina na ubora wa huduma zinazotolewa, upatikanaji wa dawa, uendeshaji na utendaji kazi wa vitengo vya hospitali na ukusanyaji wa mapato ili kugundua sehemu ambazo hospitali hizi zinaweza kuboresha na kujiongezea mapato.