![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2022/09/IMG-20220906-WA0073.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2022/09/IMG-20220906-WA0072.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2022/09/IMG-20220906-WA0074.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2022/09/IMG-20220906-WA0075.jpg)
************************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Imeelezwa kuwa Serikali hutumia kati ya sh.Milioni 200 hadi 250 kwa mwaka kwa lengo la kuwezesha bidhaa za wazalishaji wadogo kuwa na nembo ya TBS.
Hayo yalibainishwa jana Septemba 5,2022 na Meneja mahusiano na masoko wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Gladness Kaseka, wakati alipokuwa akitoa elimu kwa wajasiriamali Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza juu ya umuhimu wa matumizi ya nembo ya TBS kwenye bidhaa.
Kaseka alisema kuwa kunaumuhimu mkubwa sana kwa wajasiriamali kutumia nembo ya TBS kwenye bidhaa zao hali itakayosaidia kufanya shughuli zao kwa amani.
Alisema wanaendelea kutoa elimu kwa umma ili waweze kufahamu ni hatua gani ambazo zinatakiwa kufuatwa kwaajili ya kupata nembo ya ubora itakayowasaidia kuuza bidhaa zao kwa usalama.
Kwa upande wao wajasiriamali waliofikiwa na TBS walisema elimu hiyo itawasaidia kufanya shughuli zao kwa ufanisi.
Aidha, Shirika hilo limetoa elimu hiyo Wilaya ya Sengerema pia litaendelea na zoezi hilo katika Wilaya ya Kwimba, Misungwi, Ilemela na Magu lengo ikiwa ni kuwaelimisha wajasiriamali kuendelea kutumia nembo ya TBS kwenye bidhaa zao.