KAMISAA wa Sensa Tanzania Bara Anne Makinda,akizungumza mara baada ya kikao cha kamati ya ushauri ya kiufundi ya sensa ya tathmini ya zoezi la sensa ya watu na makazi , sensa ya majengo, na sensa ya anwani za makazi ya mwaka 2022 leo Septemba 6,2022 jijini Dodoma
Mtakwimu Mkuu wa serikali, Dk. Albina Chuwa,,akizungumza mara baada ya kikao cha kamati ya ushauri ya kiufundi ya sensa ya tathmini ya zoezi la sensa ya watu na makazi , sensa ya majengo, na sensa ya anwani za makazi ya mwaka 2022 leo Septemba 6,2022 jijini Dodoma.
……………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
KAMISAA wa Sensa Tanzania bara Anne Makinda amesema kuwa asilimia 99.9 ya kaya na 99.87 ya majengo nchini yamehesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2022.
Hayo ameyasema leo Septemba 6,2022 jijini Dodoma mara baada ya kikao cha kamati ya ushauri ya kiufundi ya sensa,Makinda amesema kuwa amesema zoezi la sensa ya watu na makazi limekamiliza rasmi na Rais Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kutangaza matokeo ya awali ya idadi ya watu Oktoba mwaka huu.
“Kati ya majengo hayo asilimia 100 ya majengo yote yaliyochukuliwa taarifa zake yamehakikiwa anwani za makazi,
Napenda kutumia fursa hii kuwashukuru wananchi wote kwa ushirikiano wenu wakati wa kutenga maeneo ya kuhesabiwa watu na wakati wa zoezi la kuhesabu watu,nawashukuru viongozi katika ngazi zote kuanzia ngazi ya Taifa hadi mtaa/kitongoji/shehia kwa jitihada zao na ushirikiano wao wakati wote wa kukamilisha awamu hii ya utekelezaji wa sensa,”amesema Makinda
Aidha amesema kuwa Serikali imehakikisha watumishi wote katika zoezi hilo wamelipwa haki zao zote Kwa mujibu wa mikataba yao ya kazi.
“Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali inathamini sana jitihada zao na watabaki kwenye kumbukumbu nzuri ya kuwa miongozi mwa vijana waliochangia maendeleo ya Nchi yetu,”alisema.
Kamisaa Makinda amesema kuwa awamu ya pili imekamilika ya utekelezaji wa sensa na sasa ni awamu ya tatu ambayo ni ya muhimu sana na inajumuisha shughuli zote za baada ya kuhesabu watu.
Kwa upande wake, Kamisaa wa Sensa kutoka Zanzibar, Balozi Mohammed Haji Hamza, amesema kuwa sensa ya mwaka huu imefanyika kwa ufanisi mkubwa kwa kutumia Tehama na wataalam wa ndani.
“katika historia ya Sensa hii imefanyikia kwa ufanisi na kutumia wataalamu wa ndani hili ni jambo la kujivunia kwani ni hatua kubwa kwa maendeleo ya nchi yetu,”alisema
Naye Mtakwimu Mkuu wa serikali, Dk. Albina Chuwa, amesema kwa Bara la Afrika ni ngumu kuhesabu kwa asilimia 100 na kwamba kimahesabu wamefikisha kiwango kilichotakiwa.
“kisayansi asilima 0.01 ni wale watakaokuja kuhesabiwa sensa ya awamu ijayo na hiyo haina hasara katika kupanga maendeleo ya Nchi,pia katika majengo Haina shida,”amesema Dk.Chuwa.