Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bi.Zuwena Jiri akifungua mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mkoani Pwani kujifunza mwongozo wa utekelezaji wa kanuni ya ushirikiano wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika leo Septemba 5,2022 Kibaha mkoani Pwani. Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bi.Zuwena Jiri akizungumza katika mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mkoani Pwani kujifunza mwongozo wa utekelezaji wa kanuni ya ushirikiano wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika leo Septemba 5,2022 Kibaha mkoani Pwani.Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt Yusuph Ngenya akikisitiza jambo wakati akizungumza katika mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mkoani Pwani kujifunza mwongozo wa utekelezaji wa kanuni ya ushirikiano wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika leo Septemba 5,2022 Kibaha mkoani Pwani. Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt Yusuph Ngenya akizungumza katika mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mkoani Pwani kujifunza mwongozo wa utekelezaji wa kanuni ya ushirikiano wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika leo Septemba 5,2022 Kibaha mkoani Pwani. Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bi.Zuwena Jiri akipata picha ya pamoja na Watendaji wa halmashauri tisa za Mkoa wa Pwani wakati wa ufunguzi wa mafunzo juu ya kujifunza mwongozo wa utekelezaji wa kanuni ya ushirikiano wa Shirika la viwango Tanzania (TBS) leo Septemba 5,2022.
(PICHA ZOTE EMMANUEL MBATILO)
*************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Pwani Bi.Zuwena Jiri amesema Serikali imeazimia kwa dhati kuendeleza biashara kwa kuhakikisha bidhaa za chakula na vipodozi zinakidhi matakwa ya viwango vya ubora na usalama.
Ameyasema hayo leo Septemba 5,2022 wakati akifungua Mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mkoani Pwani ambapo ametoa rai kwa watumishi wa serikali kuwa majukumu waliyopewa yawe chachu ya kutumikia umma kwa bidii bila ubaguzi, kuwashauri na kuwasaidia kitaalamu pale inapohitajika (tusibweteke), ili bidhaa zetu ziwe bora na salama na uchumi wetu uendelee kukua.
Amesema mafunzo hayo yamelenga kuwaelimisha watumishi kutoka ofisi za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhusu Sheria, Kanuni na miongozo inayohusika na utekelezaji wa majukumu ya ushirikiano baina ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na TAMISEMI.
Aidha amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inakuwa na mtandao mkubwa unaoshughulikia shughuli za udhibiti wa ubora na usalama wa chakula na vipodozi.
“Kwa kulitekeleza hili Serikali imeamua kuwatumia wakaguzi walio chini ya ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika shughuli za udhibiti wa bidhaa husika ili kulinda afya za watumiaji katika maeneo yao. Kwa kufanya hivi, itasaidia kuhakikisha shughuli za udhibiti zinafanyika kwa haraka na ufanisi zaidi’. Amesema RAS Zuwena.
Hata hivyo amesema mafunzo hayo ni njia muafaka ya kuleta tija zaidi katika juhudi za kuleta maendeleo katika udhibiti wa bidhaa za chakula na vipodozi katika mkoa na Taifa kwa ujumla pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wanahudumiwa kwa haraka pale inapohitajika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt Yusuph Ngenya amewataka Wafanyakazi wanaopatiwa mafunzo hayo kufanya kazi kwa weledi kwa kuwapa elimu ya kutosha wafanyabishara na wahusika wote ili huduma ziweze kuwafikia wahitaji wa chini.
“Sisi tunaenda kuwahudumia wananchi wa chini kwenye huduma za chakula na vipodozi kwa hawa wanaopatiwa mafunzo leo hivyo tuwaelimishe Wafanyabishara na siyo kusukumana polisi vile hivyo tuelimishane kama kuna mfanyabiashara atakuwa haijakidhi viwango ili aweze kukidhi viwango husika”. Amesema Ngenya.