Na Oscar Assenga,TANGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba ameupongeza Mfuko wa Self Microfinance kwa kuweza kukuza mitaji yao kutoka Bilioni 57 mwaka June 2016 hadi kufikia Bilioni 59.8 June 2022 jambo mahalo ni muhimu kwa ustawi wake.
Mgumba aliyasema hayo wakati akifungua matawi manne ya Mfuko huo ambapo alisema kwani zipo taasisi nyingi zimepewa mbegu mifuko mengine na Serikali lakini imekufa maana yake walikula lakini nyie ni taasisi inafaa zaidi na kuungwa mkono kwa kuweka mbegu zaidi kwa sababu mtaji upo salama na inaendelea kukua siku hadi siku.
Mkuu huyo alisema alifarijika zaidi kwa kuona mpango mkakati wa kuhakikisha wanaongeza matawi ili kufika mikoa yote ikiwemo kufarijika kuona Mfuko huo unatekezwa n kufanya kazi nchi mzima Tanzania bara na Visiwani.
Alisema kwamba Serikali inafahamu Mfuko wa Self ni moja ya taasisi muhimu ya fedha katika maendeleo ya sekta ya fedha na uchumi na kichocheo cha uchumi na ustawi wa maendeleo ya uchumi katika nchi.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa kipindi kilichoishia Desemba mwaka 2020/2021 mchango wa sekta ya fedha na bima katika pato la
Taifa ulikuwa kwa asilimia 3.8 utoaji wa mikopo kwa sekta binafsi ulikuwa kwa asilimia.10 ukilinganishwa kwa ukuaji asilimia 3.1 mwaka 2020 na hiyo ni rejea hali ya uchumi mwaka 2022 na hivyo kuendelea kuchochea shughuli za kiuchumi hakika mfuko umechangia kwenye ukuaji huo kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu.
“Nimesikia katia kipindi cha miesizsita mmetoa.mikopo yenye thamani ya Bilioni 16.4 kwa wakopaji 3019 na kwamba mmeanzisha huduma za mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wakati,mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali na watumishi wa umma ni jambo jema ni nyie ni taasisi mliomuelewa Rais Samia Suluhu katika kuwahudumia watanzania hususani wenye kipato kidogo na wenye mazingira magumu ya kufikia mitaji na mikopo kwenye taasisi za fedha”Alisema.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko huo,Paul Sangawe alitoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu kwa imani kubwa ambayo aliionyesha kwao kuweza kuwakabidhi jukumu hilo la kusimamia utekelezaji wa majukumu hayo huku akihaidi kwamba watafanya kazi waliopewa kwa bidii na kukutumia uwezo wao wote kuhakikisha kwamba kazi na tija ya utekelezaji wa jukumu ya Mfuko inaongezeka
Alisema ni matumaini yake kwamba ushirikiano huo utaendelea ili kuweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo na hivyo kuweza kutimiza malengo ya Mfuko huo huku akieleza mafanikio hayo yanatokana wajumbe wa bodi.
Alisema pia waliandaa mpango mkakati wa Mfuko kwa kuhakikisha wanapanua mtandao wa huduma kutoka matawi 4 hadi 12 na hivyo kuweza kufikia wateja kwa haraka zaidi ikiwemo.kuongeza huduma za mikopo kwa walengwa wa mfuko kutoka 7 hadi 10 hivyo wananchi wameweza kuchagia hivyo.
Naye kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Mudith Cheyo alisema wajasiriamali wapatao 191,865 nchini wamenufaika na mikopo kutoka Mfuko wa Self Microfinance Fund yenye thamani ya Bilioni 242 hadi kufikia June 2022 na hivyo kusaidia kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kukuza mitaji yao.
Aalisema utoaji wa mikopo hiyo ulikwenda sambamba na utoaji wa mikopo kwenye taasisi ndogo za kifedha.
Alisema pia kuanzisha huduma za mikopo ya moja kwa moja kwa muhusika ambapo ilikuwa ikiwalenga wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs),mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali wadogo na mikopo kwa watumishi wa umma .
Aidha alisema utoaji wa aina hiyo ya mikopo ni mageuzi makubwa katika kumuinua mtanzania wa kawaida kimapato na kukuza ustawi wa jamii na kuimarisha uchumi wa Taifa.
“Tunajivunia kuwa na bodi mahiri ya wakurugenzi ya Mfuko wa Self kwani chini ya usimamizi wao tumepata mafanikio mengi na ya kutia moto kwani hata idadi ya wafanyakazi imeongezeka kutoka 30 mwaka 2015 hadi 70 Sasa lakini mtandao wa matawi nao imeongezeka kufikia 12″Alisema Afisa Afisa Mtendaji huyo.
Alisema pia katika kipindi ch miezi sita kilichoishi June 2022 wameweza kutoa mikopo yenye thamani ya Bilioni 16.4 kwa wanufaika wapatao 3,091 hulu thamani ya mikopo iliyopo mikononi mwa wakopaji ikifikia Bilioni 38.4.
“Kwa ujumbe urejeshaji wa mikopo umekuwa wa kuridhisha zaidi ya asilimia 83 ya mikopo inarudi kwa wakati na Mfuko tunaendelea kuhakikisha mikopo yote inatejeshwa kwa wakati”Alisema ..
Alisema kwamba wanatambua dhamira ya Serikali ya kuanzisha taasisi hiyo na wanachukulia jukumu walilopewa kama changamoto maalumu kutokana na jukumu la msingi katika kuhakikisha kuwa watanzania wanajikwamua kiuchumi kwa kunufaika na mikopo ya masharti nafuu.
“Mfuko wa Self ulianzishwa Septemba 14 2014 na tulirithi matawi matatu kwa hiyo ufunguzi wa matawi manne mapya leo unafikisha idadi ya matawi kuwa 12 na hii ni ongezeko la matawi tisa kwa kipindi cha miezi saba kupanuka kwa mtandao wa matawi utawezesha kufikisha ya mikopo kufikisha huduma ya mikopo yenye masharti nafuu kwa watanzania wengi”Alisema
Akieleza kwamba kwa Sasa Mfuko huo una matawi Dar es Salaam,Arusha,Dodoma,Mbeya,Mwanza,Zanzibar,Kahama,Geita,Morogoro,Tanga,Mtwara na Iringa huku akieleza kwa mujibu wa mpango mkakati walionao wnatarajia kufungua matawi mengine nane ili kufikia 20 ifikapo mwaka 2026.