Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima amesema Mama Ntilie ni Kundi muhimu kwenye suala zima utoaji watoa huduma za chakula kwenye maeneo mbali mbali kwa wananchi wa kada zote hivyo Ubora wa Vyakula vyao ni muhimu kuzingatiwa kwani kwakufanya hivyo watasaidia kuokoa Afya za waliowengi
Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo Septemba 03, 2022 wakati akizindua Tamasha la Mama Ntulie kwenye Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Amesema amewapongeza Mama Ntilie hao kwa hatua hiyo waliyochukua yakuungana huku akiwahakikishia Mchakato wa Usajili wa Umoja huo.
Waziri Gwajima, amewaambia kuwa Shabaha ya Serikali ya Awamu ya Sita inayo ongoza na Mhe. Samia Suluhu Hassan nikuona suala la Usawa wa Kijinsia katika Sekta zote ikiwepo hiyo ya kiuchumi kwa Mama Ntilie Sekta kipaumbele.
“Nitumie fursa hii kuwakaribisha Ofisini kwangu Mara baada yakukamilisha michakato yote, tunapo ongelea Makundi Maalum ninyi Mama Ntilie nisehemu ya Kundi hilo hivyo wekeni Mambo yenu sawa ili tuje tuzitatue chamoto zenu kwa pamoja” Alisema Waziri Dkt Gwajima.