Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lindam Group Ltd, Zuhura Muro,akizungumza na wanawake wajasiriamali wakati wa ufunguzi wa mafunzo yanatolewa kupitia mradi wa Waendeleze ambao unafadhiliwa na Ubalozi wa Uholanzi na wanawake hao wametoka katika mikoa mbalimbali uliofanyika leo Septemba 1,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa ufunguzi wa mafunzo yanatolewa kupitia mradi wa Waendeleze ambao unafadhiliwa na Ubalozi wa Uholanzi na wanawake hao wametoka katika mikoa mbalimbali uliofanyika leo Septemba 1,2022 jijini Dodoma.
Afisa kodi kutoka kitengo cha elimu na huduma kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Peter Shewio,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha mada wakati wa ufunguzi wa mafunzo yanatolewa kupitia mradi wa Waendeleze ambao unafadhiliwa na Ubalozi wa Uholanzi na wanawake hao wametoka katika mikoa mbalimbali uliofanyika leo Septemba 1,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima General Interprises kutoka Biharamuko mkoani Kagera, Pili Makunenge,akielezea changamoto wanazokutana nazo wakati wa ufunguzi wa mafunzo yanatolewa kupitia mradi wa Waendeleze ambao unafadhiliwa na Ubalozi wa Uholanzi na wanawake hao wametoka katika mikoa mbalimbali uliofanyika leo Septemba 1,2022 jijini Dodoma.
………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lindam Group Ltd, Zuhura Muro amewashauri mambo manne wanawake wajasiriamali ikiwemo kutafuta utaalamu ili kuongeza ubora wa bidhaa wanazozalisha.
Ushauri huo ameutoa leo Septemba mosi 2022,jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa mafunzo yanatolewa kupitia mradi wa Waendeleze ambao unafadhiliwa na Ubalozi wa Uholanzi na wanawake hao wametoka katika mikoa mbalimbali.
Mkurugenzi huyo amesema wajasiriamali hao ili wawe bora wanatakiwa kutafuta utaalamu kwani biashara nyingi wanashindwa kuweka katika super market kubwa sababu ya kutokuwa na ubora.
Amesema ushauri wa pili kwa wazalishaji hao kurasimisha biashara zao kwani zitaweza kutambulika na kwa kufanya hivyo zitaweza kukua na kujulikana.
“La tatu ni kutafuta taarifa mbalimbali,kufuatana na taasisi na kujiweka katika mitandao kwani kwa kufanya hivyo utajua kinachoendelea na serikali inasema nini,”alisema Mkurugenzi huyo.
Amesema ushauri mwingine wasichukue mtaji ambao ni mkubwa na wakudidimiza biashara zao bali wanatakiwa wachukue ule unaendana na mahitaji yako na isitumike kwenye shughuli nyingine.
Mkurugenzi huyo amesema kupitia mradi huo, watawawezesha wanawake hao kupanua wigo wa masoko yao hasa nje ya nchi kwa kuendesha biashara kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vitakavyowawezesha kupenya katika masoko ya nje.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima General Interprises kutoka Biharamuko mkoani Kagera, Pili Makunenge amesema katika biashara wanakutana na changamoto mbalimbali zikiwemo kodi na tozo nyingi ambazo zinalipwa katika taasisi mbalimbali lakini zikiwa za aina moja.
Amesema changamoto nyingine ni kukosa maeneo ya uwekezaji wa viwanda kwani halmashauri nyingi hazijatenga maeneo kwa kazi hiyo.
“Tunakumbana na sera ambazo zinakuwa ni kandamizi ambazo ni kandamizi kwa sisi kina mama wajasiriamali hasa kwa sisi ambao tunaazanza biashara kama sera ya viwanda kwani hakuna sera maalum jinsi kiwanda kinavyoweza kufanya kazi,”amesema mkurugenzi huyo.
Hata hivyo anatoa wito kwa Serikali kuboresha mifumo na sera kwa ajili ya kuwawesha wanawake na wajasiriamli kuweza kufanya kazi na kujiongezea kipato
Pia, anashauri kodi kwa wajasimali zilipwe sehemu moja kwenye zimekuwa nyingi.
Kwa upande wake Afisa kodi kutoka kitengo cha elimu na huduma kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Peter Shewio amesema katika mwaka huu wa fedha Serikali imejikita katika kutoa unafuu wa kodi hasa kwenye kilimo.
Amesema imeweza kuondoa kodi kwenye vifungashio vya maziwa,mazao,mboga za majani,maua,mafuta ghafi yanayozalishwa hapa nchini na kwenye mbolea.