**********************
NJOMBE
Halmshauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imeripotiwa kutekeleza zoezi la sensa ya watu na makazi kwa zaidi ya asilimia 90 hadi usiku wa Agosti 25 mwaka huu.
Ripoti hiyo imewasilishwa na Mwenyekiti wa sensa wilaya ya ludewa kwa mkuu wa mkoa wa Njombe baada ya kufika wilayani humo na kutembelea vijiji kadhaa ili kujionea hali ya utekelezaji wa zoezi la sensa vijijini.
Kwa mujibu mwenyekiti wa sensa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere amesema hadi Sasa zaidi ya watu elfu 32 wamehesabiwa.
Wilaya hiyo inataraji kuhitimisha zoezi la kuhesabu watu siku ya tarehe 28 mwezi huu.
Tsere ambae ni mkuu wa wilaya ya Ludewa amesema licha ya mafanikio hayo makubwa lakini kumeripotiwa changamoto mbalimbali ikiwemo ya mawasiliano hususani mwambao mwa ziwa nyasa pamoja na ukosefu wa fedha za mafuta ya boti.