Mkurugenzi wa Shirika la Action for women Organization (AWO),Catherine Mongella akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha
Mmoja wa wataalamu akitoa mafunzo kwa wanawake kuhusu maswala mbalimbali ya haki za binadamu na usawa wa jinsia,uwazi na uadilifu,upimaji wa saratani ya maziwa,saratani ya kazazi,shinikizo la damu na kisukari.
………………………………….
Julieth Laizer, Arusha.
Zaidi ya Wanawake 200 kanda ya ziwa wamefikiwa na elimu juu ya kujikinga na ukatili wa kijinsia kuanzia januari hadi sasa, ambapo kupitia elimu hiyo matukio mengi ya ukatili yameweza kupungua .
Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Mkurugenzi wa Shirika la Action for Women Organization (AWO)Catherine Mongella wakati akizungumzia namna wanavyofanya kazi katika kusaidia wanawake.
Mongela amesema kuwa, kupitia elimu hiyo ya namna ya kujikinga na ukatili wa kijinsia imeweza pia kuleta hamasa kwa wanaume wengi kuweza kushiriki katika mafunzo hayo na kuweza kupata elimu zaidi na hatimaye kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo hivyo.
“Sisi tunalenga moja kwa moja kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia,kuwapa ujuzi binafsi wa namna ya kujisimamia kwa kuhakikisha wanawake wanakuwa salama na wanakuwa na uwezo wa kujilinda dhidi ya unyanyasaji wa kimwili wanaokutana nao.”amesema Mongela.
Mongela amesema kuwa,bado kuna haja ya kutolewa kwa elimu zaidi juu ya maswala ya ukatili wa kijinsia kwa makundi yote wanawake na wanaume ili mabadiliko yafanyike na kuweza kuwepo kwa matokeo chanya katika jamii husika.
“Mimi napenda kuwaasa wanawake wenzangu kuhakikisha kila mmoja anakuwa na shughuli ya kufanya kwa ajili ya kujipatia kipato ili kusaidia kuwepo kwa haki sawa katika jamii badala ya kuwa tegemezi jambo ambalo limekuwa likichangia changamoto mbalimbali. “amesema.
Aidha amewataka wanawake kujitambua na kasema ‘hapana’kwenye maswala ya ukatili wa kijinsia na ifike mahali sasa waonyeshe misimamo yao katika familia na jamii kwa ujumla.
Ameongeza kuwa,lengo la shirika hilo ni kutaka kuona jamii ambayo inaelewa na kusukuma ,kukuzwa na kulindwa kwa haki za wanawake huku wakihakikisha wanawake vijana wanawezeshwa namna ya kupanga na kutimiza malengo yao na namna ya kijithamini, usafi, SRH .
Aidha Mongela amesema kuwa,pia wamekuwa na programu ya inua vikoba ambayo inalenga kuwapa msukumo wanawake waweze kuwa na hali endelevu ya kujitegemea katika fedha kupitia VSLA au VIKOBA,huku kwa upande wa programu ya inua kilimo ikilenga kuwawezesha wanawake katika shughuli za kilimo kwa kuwapa elimu juu ya suala zima la kilimo na ufugaji wa wanyama mbalimbali.