***********************
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Leo Agosti 27,2022 kimekutana na Wafanyabiashara wa Marekani ambao ni jamii ya watu wa China kwenye kongamano kubwa la Kibiashara na Uwekezaji ambalo limefanyika katika hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kongamano hilo Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda ambaye amemwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahakikishia wafanyabiashara hao kawa Tanzania ni mahali salama pa kuja kuwekeza na wamewaandalia mazingira mazuri.
“Ni watu kutoka Marekeni ambao ni jamii ya watu wenye asili ya China na tumejaribu kuwaonyesha kuwa fursa ziko nyingi” – Mhe. Mizengo Pinda
“Yapo mambo ya msingi kwa mwekezaji yoyote ya kutaka kuja kuwekeza kwenye nchi yeyote ile, moja ni Amani na Utulivu ambapo kwa Tanzania tunamshukuru Mungu jitihads zimefanyika kwa krasi kikubwa na utuliva upo mpaka sasa”- Mhe. Mizengo Pinda
Kwa upande mwingine Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini ( TIC ) Ndg. John Mathew Mnali amesema kuwa wafanyabiashara hao wenye Makampuni Makubwa wamekuja kuwekeza kwenye sekta ya Utalii kwa kujenga hoteli za kitalii zenye hadhi ya nyota tano pamoja na kumbi kubwa za mikutano ya kimataifa na pia kuwekeza kwenye utengenezaji wa Madawa ya Binadamu.