Tanzania Kupitia Chama Cha Wahandisi wa Mitambo Ya Kuongozea Ndege (TATSEA), imekuwa mwenyeji wa mkutano wa 12 wa umoja wa vyama vya wahandisi wa mitambo ya kuongozea ndege Afrika unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 25 hadi 28 Agosti.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mkurugenzi wa huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Aron Kisaka amesema ni heshima na fahari kama taifa kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huu mkubwa wa kitaaluma.
“Wito wangu kwenu ni kila mmoja wenu afanye majukumu yake kwa uzalendo wa nchi yake huku akitambua kuwa amebeba thamana ya bara letu la Afrika, hivyo maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga ya afrika yapo mikononi mwenu”.Amesena Mhandisi Kisaka
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza S. Johari amepongeza jitihada zinazofanywa na Umoja huo (IFATSEA) katika kuzianisha, kuzikabili na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazoikabili taaluma hii muhimu katika sekta ya usafiri wa anga.
“Nawasihi mdumishe ushirikiano baina yenu na hasa wa kubadilishana ujuzi wa teknolojia kwani inaenda ikibadilika kila uchwao”.Amesema Hamza S. Johari
Mwenyeji wa mkutano huo, rais wa chama cha wahandisi wa mitambo ya kuongozea ndege Tanzania (TATSEA) Bw. Francis Chale amewakaribisha wajumbe wote na kuwahakikishia kuwa Tanzania ni sehemu sahihi na salama ya mkutano huu wenye tija na maana kubwa kwa maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga Afrika na duniani kwa ujumla.
Mkutano huu wa 12 unafanyika jiji I Dar Es Salaam,Tanzania ikiwa ni baada ya ule wa 11 uliofanyika jijini Abuja, Nigeria mwaka 2019 na kutofanyika kwa miaka miwili kufuatia changamoto za janga la UVIKO 19.
Mkurugenzi wa huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Aron Kisaka akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa 12 wa umoja wa vyama vya wahandisi wa mitambo ya kuongozea ndege Afrika(IFATSEA) kinachofanyika ijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 25 hadi 28 Agosti 2022. Mhandisi Aron Kisaka alifungua mkutano huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Gabriel Migile.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S. Johari akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 12 wa umoja wa vyama vya wahandisi wa mitambo ya kuongozea ndege Afrika(IFATSEA) uliofunguliwa na Mkurugenzi wa huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Aron Kisaka kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Gabriel Migile.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Ghana(GCAA), Daniel Acquah akitoa salamu kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo wakati wa ukufungua mkutano wa 12 wa umoja wa vyama vya wahandisi wa mitambo ya kuongozea ndege Afrika(IFATSEA) kinachofanyika ijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 25 hadi 28 Agosti 2022.
Rais wa Chama cha Wahandisi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege Tanzania(TATSEA), Mhandisi Francis Asante Chale akizungumza kuhusu namna walivyojiapnga kusimamia mkutano huo kama wenyeji wakati wa ukufungua mkutano wa 12 wa umoja wa vyama vya wahandisi wa mitambo ya kuongozea ndege Afrika(IFATSEA) kinachofanyika ijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 25 hadi 28 Agosti 2022.
Katibu Mtendaji wa Umoja wa vyama vya wahandisi wa mitambo ya kuongozea ndege Afrika(IFATSEA), Frank Koffi Apeagyei akizungumza wakati wa mkutano wa 12 wa umoja wa vyama vya wahandisi wa mitambo ya kuongozea ndege Afrika(IFATSEA) kinachofanyika ijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 25 hadi 28 Agosti 2022.
Baadhi ya wanachama wa umoja wa vyama vya wahandisi wa mitambo ya kuongozea ndege Afrika(IFATSEA) pamoja na wadau wa Sekta ya Anga wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mkurugenzi wa huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Aron Kisaka aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Gabriel Migile wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 12 wa IFATSEA unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 25 hadi 28 Agosti 2022.
Mkutano ukiendelea
Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Aron Kisaka akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S. Johari, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Ghana(GCAA), Daniel Acquah pamoja na baadhi ya wanachama wa umoja wa vyama vya wahandisi wa mitambo ya kuongozea ndege Afrika(IFATSEA) pamoja na wadau wa Sekta ya Anga mara baada ya kufungua mkutano wa 12 wa IFATSEA.
Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Aron Kisaka akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa 12 wa umoja wa vyama vya wahandisi wa mitambo ya kuongozea ndege Afrika(IFATSEA) unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 25 hadi 28 Agosti 2022.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S.Johari akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Aron Kisaka kufungua mkutano wa 12 wa umoja wa vyama vya wahandisi wa mitambo ya kuongozea ndege Afrika(IFATSEA) unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 25 hadi 28 Agosti 2022.