Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka Saini katika kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema wakati alipofika Nyumbani kwa Marehemu Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Agosti 2022. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Bi. Doreen Kimbi ambaye ni mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema wakati alipofika kutoa pole nyumbani kwa marehemu Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwafariji wanafamilia, viongozi na wanachama wa TLP alipofika msibani nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiongoza sala ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema walipofika msibani nyumbani kwa marehemu Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam.
………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wamefika salasala Jijini Dar es salaam nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema ili kutoa pole na kuifariji familia, ndugu , jamaa na marafiki kufuatia kifo cha kiongozi huyo aliyefariki tarehe 21 Agosti 2022 katika hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Akiwa nyumbani hapo, Makamu wa Rais amewapa pole wana familia na kuwaomba kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu. Makamu wa Rais amesema Marehemu Mrema alikuwa ni kiongozi mkweli na mzalendo kwa taifa ambapo wakati wote alitetea maslahi ya nchi. Amesema taifa limepoteza kiongozi aliyetumikia vizuri nafasi zote alizowahi kuongoza katika uhai wake.