Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihojiwa na kutoa majibu ya dodoso kuu la Sensa ya Watu na Makazi kwa Karani wa Sensa Amina Mwambe wakati alipokuwa akihesabiwa katika Makazi yake ya Kijiji cha Nandagala, Ruangwa Mkoani Lindi Agosti 23, 2022 wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema amefarijika na jinsi zoezi la sensa ya watu na makazi lilivyoanza mwaka huu na kupokelewa katika maeneo mbalimbali nchini.
“Kwa kweli nina faraja sana kwamba kati ya sensa zilizofanyika hapa nchini, hii ya mwaka huu Watanzanua wameipokea vizuri na wamehamasika sana,” amesema.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Agosti 23, 2022) mara baada ya kumaliza kuhojiwa na karani wa sensa nyumbani kwake kijiji cha Namahema, kata ya Nandagala, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.