Karani akiendelea na zoezi la sensa katika Kijiji cha Wachawaseme wilayani Mlele
************************
Na Zillipa Joseph, Katavi
Karani wa Sensa Kata ya Majimoto Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi mwalimu Kenan Kasekwa amevamiwa usiku wa kuamkia leo na kuporwa kishikwambi cha kutunzia kumbukumbu za Sensa.
Akithibitisha tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Catherine Mashala amesema karani huyo ambae ni mwalimu alivamiwa na mtu ambae alivunja kitasa na kuingia chumbani kisha kubeba kifaa hicho,fedha kiasi cha sh 760,000/-,radio na vitu vingine.
“Inavyoonekana mwizi alipuliza dawa ya kuwalaza usingizi yeye na familia yake, yule mwizi alingia chumbani akabeba begi, kishikwambi, na fedha alizozikuta, simu na radio aina ya sabufa”alisema Mashala
Bi. Mashala ameiambia Full Shangwe kuwa,baada ya tukio hilo alitoa taarifa kituo cha Polisi ndipo Polisi walipofuatilia na kufanya msako na kumkamata mtuhumiwa na mpaka taarifa hii inaruka hewani mtuhumiwa anaendelea na mahojiano zaidi.
Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya ya Mlele Filberto Sanga amesema zoezi la sensa ya watu na makazi limeanza vizuri na linaendelea vizuri
Naye mratibu wa sensa halmashauri ya Mlele Deo Johanes amesema Wana makarani wa kutosha zaidi ya 150 ambapo zoezi linaenda vizuri