Mhe. Prof. Juma ameshiriki zoezi hilo kwa kuhesabiwa na Karani wa Sensa, Bi. Yvonne Ngakongwa alipomtembelea nyumbani kwake Oysterbay barabara ya Kajificheni jijini Dar es Salaam.
Hivi karibuni, Mhe. Jaji Mkuu alisema kuwa, “Kwa upande wa Mahakama, Sensa ni zoezi muhimu sana kwa sababu inatupa idadi sahihi ya watu itakayosaidia kuboresha zaidi huduma za utoaji haki kwa wananchi.”
Mhe. Prof. Juma alisema hivyo, na kutoa rai kwa wananchi kushiriki katika zoezi hilo muhimu kwa uboreshaji wa huduma za utoaji haki na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
MATUKIO KATIKA PICHA JAJI MKUU WA TANZANIA, MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA ALIPOSHIRIKI ZOEZI LA SENSA.
Karani wa Sensa, Bi.Yvonne Ngakongwa akiendelea na mahojiano na Mkuu wa Kaya ya familia ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (hayupo katika picha).
Mahojiano yakiendelea kati ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ambaye ni Mkuu wa Kaya na Karani wa Sensa, Bi. Yvonne Ngakongwa (kulia).