Mwenyekiti wa ccm kata ya Olorieni,Sostenes Macha mwenye (shati la njano )akikabithi zawadi ya mbuzi kwa washindi wa kwanza katika bonanza hilo la kuhamasisha sensa kwa madereva bodaboda lililofanyika kata ya Olorieni jijini Arusha.
Mkuu wa wilaya ya Arusha, Said Mtanda akizungumza katika zoezi hilo la kuhamasisha sensa kwa madereva bodaboda lililofanyika katika kata ya Olorieni jijini Arusha
Katibu siasa na uenezi kata ya Olorieni ambaye pia ni Mkurugenzi wa Waifuraha Polyclinic,dokta Frank Chacha akizungumza katika bonanza hilo jijini Arusha.
Julieth Laizer ,Arusha.
Arusha.Zikiwa zimebakia siku moja kuelekea zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika kesho agosti 23 ,2022 ,Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Said Mtanda amewataka madereva bodaboda jiji la Arusha kuhamasisha zoezi hilo ili vijana wenzao waweze kushiriki kikamilifu na kutoa ushirikiano katika zoezi hilo.
Ameyasema hayo jijini Arusha katika kata ya Olorieni wakati akizungumza na madereva bodaboda wa kata hiyo katika fainali ya bonanza la mbuzi lililolenga kuhamasisha zoezi la sensa.
Mtanda amesema kuwa,zoezi hilo lililoandaliwa na viongozi wa chama cha mapinduzi kata ya Olorieni ni jambo zuri na linapaswa kuigwa kwani waendesha bodaboda wana mchango mkubwa sana wa kuhamasisha zoezi la sensa hususani kwa vijana wenzao kutokana na kundi kubwa wanalokutana nalo.
“Nawapongeza viongozi wa chama cha mapinduzi kata hii kwa namna ambavyo wameona umuhimu wa kuandaa bonanza hili la kuhamasisha zoezi la sensa kwa waendesha bodaboda ili waweze kutoa ushirikiano na kufanikisha zoezi hilo “amesema Mtanda.
Amesema kuwa, swala la sensa ni la kila mmoja watu kwani kazi yake kubwa ni kusimamia sensa kwa hamasa ili lifanyike vizuri .
Mtanda amewataka madereva bodaboda kuwa waangalifu katika kazi yao hulu wakifuata sharia na taratibu zilizopo ili kuepusha ajali sa barabarani.
Naye Mwenyekiti ccm kata ya Olorieni,Sostenes Macha amesema kuwa bonanza hilo lilianza alhamisi huku lengo la bonanza hilo likiwa ni kuhamasisha swala zima la sensa ili madereva hao waweze kutoa ushirikiano katika maeneo mbalimbali na kwa kufanya hivyo ni kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika swala zima la kuhamasisha sensa.
Macha amesema kuwa, bonanza hilo lilishirikisha timu nne za madereva bodaboda ambapo mshindi aliweza kupatiea zawadi ya mbuzi .
Naye Katibu siasa na uenezi kata ya Olorieni ambaye pia ni Mkurugenzi wa Waifuraha Polyclinic ,Frank Chacha amewataka madereva hao kuhamasisha vijana wenzao kushiriki katika zoezi hilo kwa manufaa yao mwenyewe hali ambayo itairahisishia serikali kupanga mipango yake ya maendeleo.
“Tumekuwa tukifanya mabonanza kama hayo mara kwa mara ila la leo ni kwa ajili ya kuhamasisha zoezi zima la sensa ikiwa ni sehemu mojawapo ya kumuunga mkono Rais Samia katika swala zima la sensa. “amesema Chacha.