Mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule akimkabidhi hati miliki ya kimila mmoja ya wanufaika wa MKURABITA kutoka mtaa wa lumwagi
Mpango wa urasimishaji biashara na ardhi kwa wanyonge MKURABITA umekabidhi hati za kimila zaidi ya 1300 kwa wakazi wa mtaa wa lumwagi kata ya upendo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kama moja ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi pamoja na kuondokana na migogoro mbalimbali ya ardhi.
Akikabidhi hati hizo mkuu wa wilaya yaMufindi Saad Mtambule amesema upatikanaji wa hati hizo utasaidia kuondokana na migogoro ya ardhi lakini pia kujikwamua kiuchumi kwa hati kutumika kama dhamana katika kuomba mikopo kwa taasisi mbalimbali za kifedha.
‘’Sasa mmekabidhi hati mnayonafasi ya kwenda kwenye mabenki yetu na kupatiwa mkoapo utakaowawezesha kujiendeleza katika kufanya biashara lakini pia kulima kisasa na kujipatia kipato kitakachosaidia kuinua maisha yenu ya kila siku na niseme tu taasisi mbalimbali za kifedha ziko hapa kazi imebaki kwenu’’Saad Mtambule Mkuu wa wilaya ya Mufindi.
Lakini naye mratibu wa MKURABITA Dkt.Seraphia Mgembe amesema muitikio umekuwa mkubwa tofauti na makadilio yaliyowekwa kutokana na watu wa eneo hilo kujitokeza kwa wingi na kupimiwa viwanja vyao na kupewa hati.
‘’Kwa kweli sisi tulijipanga kupima viwanja 1000 lakini ni tumepima viwanja 13005 yaan asilimia 130 ya lile lengo letu nah ii yoote imewezekana kwa ajili ya muitikio wa wananchii na chakushangaza tumetengeneza invoice 752 kwa ajili ya watu kulipia lakini 680 zimelipiwa na hilo ni mafanikio makubwa’’Dkt.Seraphia Mghembe.
Theodora Sanga ni mmoja ya wanufaika waliopimiwa kiwanja na kukabidhiwa hati miliki ya kimila alisema kuwa kwa sasa wataondokana na migogoro na ikiwezekana wataitumia hati hiyo katika kuendeleza shamba ambalo amepanda miti