Wananchi wa Wilaya ya Temeke waliojitokeza kwenye Bonanza la hitimisho la hamasa ya Sensa ya watu na Makazi lililofanyika katika viwanja vya Zakiem Mbagala Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwegelo akiongoza matembezi maalumu katika kuhamasisha sensa ya makazi na watu leo katika viwanja vya Zakiem Mbagala Jijini Dar es Salaam Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe Jokate Mwegelo katikati akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Ndg. Ndg. Elihuruma Mabelya ( Kulia ) na Mbunge wa Jimbo la Mbagala Mhe. Abdallah Chaurembo ( Kushoto ) wakiwa kwenye Bonanza maalum la kuhamasisha Sensa ya Watu na Makazi. Wananchi wa Wilaya ya Temeke waliojitokeza kwenye Bonanza la hitimisho la hamasa ya Sensa ya watu na Makazi lililofanyika katika viwanja vya Zakiem Mbagala Jijini Dar es Salaam
**********************
NA MWANDISHI WETU
Katika kuelekea siku ya Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23,2022, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwegelo amewahamasisha Wananchi wa Wilaya hiyo kujitokeza na kushiriki kwa wingi ili kuipatia fursa serikali kuweka mikakati muhimu katika Taifa.
“Hiyo ni siku ya mapumziko mahususi kutoa nafasi kwa Wananchi wote kuweza kushiriki bila kuwa na sabbabu zingine kwenye zoezi hili la sensa” amesema DC Jokate
“Nawaomba Wananchi wenzangu wa Temeke tume watulivu, tuonyeshe ushirikiano kwa Makarani watakaofika kwenye maeneo yetu” amesema DC Jokate
Amesema hayo leo kwenye Bonaza kutwa lililofanyika katika viwanja vya Zakhiem Mbagala vilivyopo katika wilaya hua Temeke na kuhudhuriwa na Viongozi Mbalimbali wakiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Naibu Meya na Madiwani wa wilaya hiyo na Baadhi ya Wasanii wa Bongo Fleva Juma Nature, Yamato Band na wengineo.
Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Ndg. Elihuruma Mabelya amezidi kuwasisitizia Wananchi wa wilaya hiyo kuwaitiske zoezi la Sensa ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
“Zoezi la Sensa ni muhimu, hamasa imefanyika na leo ni hitimisho la hamasa ambayo Mkuu wetu wa Wilaya ameifanya Usiku na mchana. Wilaya yetu ina mitaa 142 na kata 23 ambayo inahitaji maendeleo” amesema Mabelya.
Tukumbuke siku ya Tarehe 23 mwezi huu wa nane mwaka 2022 itakuwa sensa ya makati na watu itakayofanyika Nchi nzima na siku hiyo itakuwa ni siku ya mapumziko kitaifa.