Na Jumbe Ismailly ITIGI
MASHINDANO ya ligi kugombea kombe la tembo, ’’TEMBO CUP 2022’’
yanayopendelea katika Halmashauri ya Itigi, wilayani Manyoni,Mkoani Singida
yameingia katika hatua ya nusu fainali,ambapo timu za Kitaraka FC,Doroto
FC,Sanjaranda FC na Muhanga Fc zimefanikiwa kutinga hatua hiyo.
Katika mchezo uliopigwa katika Viwanja vya Shule ya Msngi Kitaraka,Timu ya
Doroto FC ilipata goli la kuongoza katika dakika 26 lililofungwa na Karimu
Mrinja na Kitaraka FC walipata goli la kusawazisha katika dakika ya 63 mfungaji
akiwa Bashiru Ally na kuzifanya timu hizo kutoka sare ya kufungana goli 1 kwa
1.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Lucas Alfayo akisaidiwa na
washika vibendera Marco Damasi na Paschal Mapalala,ndipo baada ya matokeo hayo
mwamuzi wa mchezo huo alilazimika kutumia sheria inayozitaka timu hizo kupiga
mpira ya adhabu na ndipo Daroto FC walipata kona 4 dhidi ya kona 3 za Kitaraka
FC na hivyo kuiwezesha Doroto FC kutinga fainali na timu ya Muhanga FC.
Hata hivyo katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa shule ya msingi Ipande
uliozishirikisha timu za Muhanga FC na Smart boy FC,timu hizo zilitoka kwa sare
ya kufungana goli 1 kwa 1 na hivyo kuingia kwenye hatua ya penalti na ndipo
Muhanga FC waliibuka na ushindi wa jumla ya goli 3 kwa 1walilopata Sanjaranda.
Kufuatia matokeo hayo mchezo wa fainali kwa timu za Muhanga FC na Doroto FC
unatarajiwa kufanyika katika uwanja wa michezo wa shule ya msingi Doroto ili
kupata bingwa wa mashindano haya huku timu za Sanjaranda FC na Smart boy FC
zikichuana kumpata mshindi wa tatu.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mchezo kati ya Muhanga na Smart
boy,Diwani wa Kata ya Ipande,Kedmon Mpondo pamoja na mambo mengine alitumia
fursa hiyo kulishukuru shirika la STEP kwa ufadhili wake wa kuandaa mashindano
hayo kwa mwaka wa nne mfululizo hivi sasa pamoja na kuwasaidia kuunda vikundi
vya wajasiriamali.
Diwani huyo mpenda michezo alifafanua kwamba licha ya kupatiwa elimu juu ya
kuishi vizuri na mnyama tembo,vile vile watakuwa tayari kuhakikisha tembo
anakuwa ni rafiki na binadamu kwa kuhakikisha anapata ulinzi wa kutosha katika
maisha yake.
‘’Na sisi kama kata ya Ipande mashindano haya yametunufaisha sana kwani
vijana wanakuza vipaji na hatimaye timu yetu ya Muhanga imeingia fainali na
kesho itaenda kucheza Doroto.’’alisisitiza diwani huyo kijana na mpenda
michezo.
Mashindano hayo yaliyozishirikisha jumla ya timu 20 kutoka katika kata
zilizopo kwenye hifadhi ya Muhesi,yameandaliwa na Shirika lisilokuwa la
kiserikali (STEP) limalojishughulisha na uhifadhi wa tembo nchini.