Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwatunuku Shahada ya Uzamivu Wahitimu kutoka Skuli wajati wa Shere za Mahafali ya 8 katika Taasisi hiyo Agosti 18,2022 katika Kampasi ya Tengeru, Arusha.
Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Dkt. Mohammed Gharib Bilal ( hqyupo katika picha ) akiwatunuku Shahada ya Umahili Wahitimu kutoka Skuli wajati wa Shere za Mahafali ya 8 katika Taasisi hiyo Agosti 18,2022 katika Kampasi ya Tengeru ,Arusha.
Mlau wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Jerome Buza akisoma risala wakati wa mahafali ya 8 ya kuwatunuku Shahada ya Umahili na Uzamivu wahitimu kutoka Taasisi hiyo Agosti 18,2022 katika Kampasi ya Tengeru ,Arusha
Mlau Profesa Jerome Buzza wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela akiongoza maandamano mara baada ya kuhitimisha Mahafali ya 8 ya kutunuku Shahada ya Umahili na Uzamivu wahitimu wa Taasisi hiyo Agosti 18,2022 katika Kampasi ya Tengeru Arusha.
……………………………………
Wanawake wahimizwa kupenda kusoma masomo ya Sayansi, Uhandisi na Hisabati Ili kuwa na wasomi wengi wanawake katika sekta ya uchumi.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohammed Gharib Bilal Agosti 18, 2022 Jijini Arusha, wakati wa mahafali ya 8 ya kutunuku Shahada ya Umahili na Uzamivu kwa wahitimu 131 wa Taasisi hiyo.
Dkt. Bilal ameeleza kuwa, licha ya Serikali kuweka hamasa zaidi kwa wanawake kupenda masomo ya Sayansi, Hisabati na Uhandisi lakini bado mwamko sio mkubwa sana na kuwataka wanawake kutokuogopa kusoma masomo hayo ili kuongeza idadi ya wasomi wanawake katika sekta hizo.
“Uchumi wa nchi unakua kwa kasi, sasa ni zamu ya wanawake kupenda masomo hayo pamoja na kuwapa motisha watoto wa kike kupenda masomo hayo ili kuwa na wataalam wengi zaidi” amesema Dkt. Bilal
Naye Makamu Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela(NM -IST), Profesa Emmanuel Luoga amewataka wahitimu hao kuwa chachu ya maendeleo ya nchi na binafsi kwa kufanyia kazi yale yote walivyojifunza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi hiyo, Profesa Joseph Buchweishaija amesema Taasisi ya Nelson Mandela iimekuwa mstari wa mbele katika kuibua watafiti na wabunifu mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa suluhisho mbalimbali za kisera na kiutendaji kupitia tafiti wanazofanya.
Vilevile Profesa Buchweishaija ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kufanikisha ujenzi wa Bweni la wanafunzi ambalo ni la kipekee kwa kuwa na vyumba maalum kwa ajili ya wanafunzi wanawake wenye watoto wadogo hivyo kuwapa fursa ya kusoma wakiwa na watoto wao.
Katika mahafali hayo ya 8 jumla ya wahitimu 131 wametunukiwa Shahada za Umahili na Uzamivu ,huku Shahada ya Umahili ( Master’s) wakiwa 103 na Shahada ya Uzamivu (28) wakiwa 28.