Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiweka jiwe la msingi ujenzi wa Madarasa na maabara katika shule ya sekondari Maria De Mattias inayomilikiwa na Makao ya Watoto Kijiji cha Matumaini kilichopo Dodoma wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 20 ya Kijiji cha Matumaini yaliyofanyika leo Agosti 17,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akishiriki ujenzi wa Madarasa na maabara katika shule ya sekondari Maria De Mattias inayomilikiwa na Makao ya Watoto Kijiji cha Matumaini Dodoma wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 20 ya Kijiji cha Matumaini yaliyofanyika leo Agosti 17,2022 jijini Dodoma.
Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya,akishiriki ujenzi wa Madarasa na maabara katika shule ya sekondari Maria De Mattias inayomilikiwa na Makao ya Watoto Kijiji cha Matumaini Dodoma wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 20 ya Kijiji cha Matumaini yaliyofanyika leo Agosti 17,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwekajiwe la msingi ujenzi wa Madarasa na maabara katika shule ya sekondari Maria De Mattias inayomilikiwa na Makao ya Watoto Kijiji cha Matumaini kilichopo Dodoma wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 20 ya Kijiji cha Matumaini yaliyofanyika leo Agosti 17,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wanajumuiya wa Makao ya Watoto Yatima na wasiojiweza wa Kijiji cha Matumaini wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 20 ya Kijiji cha Matumaini yaliyofanyika leo Agosti 17,2022 jijini Dodoma.
Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 20 ya Kijiji cha Matumaini yaliyofanyika leo Agosti 17,2022 jijini Dodoma.
Muasisi wa Kijiji cha Matumaini Sr. Rosaria ASC,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 20 ya Kijiji cha Matumaini yaliyofanyika leo Agosti 17,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Shirika Sr. Nadia Coppa ,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 20 ya Kijiji cha Matumaini yaliyofanyika leo Agosti 17,2022 jijini Dodoma.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Msaidizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Baraka Makona,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 20 ya Kijiji cha Matumaini yaliyofanyika leo Agosti 17,2022 jijini Dodoma.
Sr. Lucina Johannes SCA Mkuu wa Kanda ya Tanzania Masista Waabuduo,akitoa utambulisho wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 20 ya Kijiji cha Matumaini yaliyofanyika leo Agosti 17,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akitoa zawadi kwa wanajumuiya ya makao ya kulea watoto wa Kijiji cha Matumaini kwa mchango wao katika malezi ya watoto wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 20 ya Kijiji cha Matumaini yaliyofanyika leo Agosti 17,2022 jijini Dodoma.
Kikundi cha Makunga cha wanafunzi wa Shule ya Msingi Maria De Mattias ,wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 20 ya Kijiji cha Matumaini yaliyofanyika leo Agosti 17,2022 jijini Dodoma.
………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,amewataka wamiliki wa makao ya kulea watoto kuwaandaa kisaikolojia watoto kupitia huduma zinazotolewa na mipango ya kuwaondoa makaoni.
Hayo ameyasema leo Agosti 17,2022 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya Miaka 20 ya makao ya watoto yatima wasiojiweza Kijiji cha Matumaini Jijini Dodoma yaliyofanyika leo Agosti 17,2022
Waziri Dkt Gwajima amesema mchakato huo usipofanyika ipasavyo husababisha watoto kuona Makao ni nyumbani kwao na sehemu ya kudumu, hivyo kulelewa hadi utu uzima na mara nyingi wakitoka makaoni hushindwa kujitegemea, kuishi katika familia zao au kutengamanishwa katika jamii.
“Kupitia siku hii muhimu, nawaagiza wamiliki na waendeshaji wa Makao nchini kuhakikisha kila mtoto anayepokelewa makaoni anaandaliwa mpango wa huduma unaojumuisha mpango wa kutoka Makaoni na taarifa zote zihifadhiwe katika jalada la mtoto” amesema Waziri Dkt. Gwajima.
Amewaagiza pia Maafisa Ustawi wa Jamii kote nchini kuhakikisha agizo hili linatekelezwa katika maeneo yao na Msajili wa Makao, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI wafanye ufuatiliaji ipasavyo.
Amesema idadi ya Watoto 145 wanaolelewa katika makao hayo ni sehemu ya Watoto 24,454 wanaolelewa katika makazi 324 yaliyosajiliwa nchini yakiwemo makao mawili ya Serikali ya Kurasini Dar es Salaam na Kikombo Dodoma.
“Hata hivyo malezi ya watoto makaoni ni suluhisho la mwisho wakati sababu zilizochangia zikiwa zinafanyiwa kazi” alisema Waziri Gwajima.
Aidha, Waziri Dkt Gwajima ameahidi kushirikiana na Mamlaka zinazohusika kusaidia ufumbuzi wa changamoto ya utozwaji kodi katika miradi iliyobuniwa ambayo inaathiri utumiaji wa mapato katika kukidhi mahitaji mbalimbali ya watoto wanaolelewa makaoni hapo.
Akisoma risala ya makao hayo, msimamizi wa Utawala katika Kijiji cha Matumaini Baltazar Sungi amesema makao hayo yaliyoanzishwa mwaka 2022 yanatumia mfumo wa familia kwa wanakaya kujitolea kuwatunza
watoto hao.
“Hivi sasa watoto wanaohudumiwa hapa ni 145, 62 wavulana na 85 ni wasichana kutoka sehemu mbalimbali Tanzania na walezi 26 wa kujitolea” alisema Bartazar.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya ameiomba Serikali makao hayo kutambuliwa kama watoa huduma za hisani ili wapunguziwe baadhi ya kodi.
Kwa upande wa mmoja wa wanufaika waliolelewa katika makao hayo pamoja na mlezi wake Elizabeth Gamaka wameshukuru kwa uwepo makao hayo na kuwaasa wazazi wanaotelekeza watoto kuacha tabia hiyo.
Maadhimisho hayo wameenda sambamba na harambee ya ujenzi wa baadhi ya Majengo kwenye Kijiji hicho ambapo Serikali kupitia Wizara imechangia jumla ya shilingi Milioni tano.