WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati akitangaza timu ya Wataalamu ya kufanya utafiti fuatilizi wa wahitimu wa mafunzo ya ufundi VETA) kwa wadau wa elimu wa mapitio ya maoni juu ya uboreshaji wa sera ya elimu na mabadiliko ya mitaala ya elimu msingi leo Agosti 16,2022 jijini Dodoma.
WADAU wa Elimu wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati akitangaza timu ya Wataalamu ya kufanya utafiti fuatilizi wa wahitimu wa mafunzo ya ufundi VETA) kwa wadau wa elimu wa mapitio ya maoni juu ya uboreshaji wa sera ya elimu na mabadiliko ya mitaala ya elimu msingi iliyofanyika leo Agosti 16,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Francis Michael,akizungumza wakati wa kutangazwa kwa timu ya Wataalamu ya kufanya utafiti fuatilizi wa wahitimu wa mafunzo ya ufundi VETA) kwa wadau wa elimu wa mapitio ya maoni juu ya uboreshaji wa sera ya elimu na mabadiliko ya mitaala ya elimu msingi iliyofanyika leo Agosti 16,2022 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo,akizungumza wakati wa kutangazwa kwa timu ya Wataalamu ya kufanya utafiti fuatilizi wa wahitimu wa mafunzo ya ufundi VETA) kwa wadau wa elimu wa mapitio ya maoni juu ya uboreshaji wa sera ya elimu na mabadiliko ya mitaala ya elimu msingi iliyofanyika leo Agosti 16,2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Timu hiyo, Dk. Hamis Mwinyimvua,akizungumzia jinsi watakavyofanya utafiti huo leo Agosti 16,2022 jijini Dodoma
…………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,ameunda timu ya Wataalamu ya kufanya utafiti fuatilizi wa wahitimu wa mafunzo ya ufundi kutoka Vyuo vya Ufundi Stadi nchini (VETA), ili kusaidia maboresho ya mitaala nchini.
Timu hiyo inaongozwa na Dkt. Hamisi H. Mwinyimvua ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) na wajumbe wanne ambao ni Prof. Deograsias P. Mushi Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Dkt. John Chegere Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Dkt. Claude Maeda Mhadhiri kukota Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Dkt. Ibrahim Kadigi Mhadhiri kukota Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
Akitangaza timu hiyo ya Wataalamu leo Agosti 16,2022 jijini Dodoma kwa wadau wa elimu wa mapitio ya maoni juu ya uboreshaji wa sera ya elimu na mabadiliko ya mitaala ya elimu msingi.
Waziri Mkenda amesema kwa sasa msukumo mkubwa uko katika masuala ya ujuzi hivyo taarifa itakayotokana na utafiti huo itakuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha elimu inayotolewa inatoa ujuzi utakaowezesha wahitimu kuwa na ujuzi utaokawezesha kuajiriwa ama kujiajiri.
“Tunafanya ufuatiliaji ili tutakapopitia mitaala ya mafunzo ya Ufundi Stadi tujue tunakwenda vipi kwa kuwa tutakuwa tumefahamu mahitaji ya soko na tunakoenda tunataka wahitimu hawa wakimbiliwe na waajiri ” amesema Prof. Mkenda.
Waziri Mkenda amesema kwa kuelewa kuwa wahitimu wa mafunzo ya VETA wameongezeka kutoka 179,930 mwaka 2016 hadi 295,446 mwaka 2020, na utafiti wa mwisho wa aina hii ulifanyika mwaka 2018 kwa waajiriwa wa 2010 – 2015, malengo ya Utafiti wa Ufuatiliaji unaofanywa na Timu hiyo itakuwa ni Kujua walipo na wanafanya shughuli gani wahitimu wa mafunzo ya VETA baada ya kuhitimu masomo yao (waliohitimu 2017 – 2021).
”Kulinganisha na mahitaji ya soko la ajira na uzalishaji wa wahitimu wa VETA (demand vs supply of graduates in the labour market), Kujua kama ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira unaendana na ujuzi unaofundishwa na vyuo husika, na Kujua kama kuna waajiri wasioajiri wahitimu wa VETA na sababu zake.”amesisitiza
Aidha Prof. Mkenda amewataka wale wote watakaohusika katika utafiti huo kutoa ushirikiano kwa kuwa lengo ni kuboresha na kufikia malengo makubwa ya Taifa ambayo ni kutoa elimu yenye ujuzi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara hiyo, Dk.Francis Michael, amesema kuwa Wizara inaendelea na utaratibu wa ushirikishwaji katika kuboresha sekta ya elimu nchini.
Naye Mwenyekiti wa Timu hiyo, Dk. Hamis Mwinyimvua amesema utafiti utakaofanyika utahusisha wahitimu wa VET wa kuanzia mwaka 2017 hadi 2021 waliopata elimu hiyo kupitia mifumo mbalimbali ya mafunzo hayo.
Amesema utafiti huo utafanyika nchi nzima na utahusisha wahitimu wa vyuo mbalimbali vya Serikali na binafsi, waajiri walioajiri wahitimu wa VET na wale ambao hawaja ajiri wahitimu hao, walimu na wakufunzi wa vyuo hivyo, Mabaraza ya Kisekta, Chama cha Waajiri nchini (ATE) , Shirkisho la Sekta Binafsi (TPSF) na wadau wengine.
Amesema baadhi ya maeneo watakayoangalia katika utafiti huo ni iwapo wahitimu hao wameajiriwa, namna wanavyotumia utaalamu wao katika kazi wanazotekeleza, changamoto na kama ujuzi walioupata unaendana na soko la ajira.
“Kwa ujumla utafiti unalenga kutathmini athari chanya au hasi za muda mrefu kwa programu mbalimbali za elimu ya ufundi stadi ili kupata taarifa zitakazo wezesha kuboresha mitaala na mazingira ya utoaji elimu na mafunzo hayo pamoja na kubaini changamoto za wahitimu hao kwenye soko la ajira,” amefafanua Dkt. Mwinyimvua.