*************************
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani,alhaj Abubakari Kunenge ameeleza mkoa wa Pwani Ni eneo salama kwa ajili ya fursa ya uwekezaji na viwanda ,hivyo amewaasa wawekezaji wasisite kwenda kuwekeza Mkoani humo .
Amewakaribisha na kuwaeleza kuwa Mkoa wa Pwani ni Mahali sahihi kwa Uwekezaji Nchini kwani umesheheni maeneo ya kutosha yaliyotengwa kwa ajili ya kuwekeza na viwanda pamoja na miundombinu iliyo rafiki kwa ajili Yao.
Kunenge amehamasisha wawekezaji kujitokeza zaidi baada ya kukutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa Tanzania Nchini Saudi Arabia Ali J. Mwadini aliyeambatana na Mwekezaji Alghmlas Abdalah Kutoka Reyadh Nchini Saudi Arabia.
Kunenge amewaeleza kuwa Mkoa huo unafursa nyingi za Uwekezaji kwenye Sekta ya Viwanda, Uvuvi, Kilimo Utalii,na Mifugo.
“Pia upo Eneo la Kimkakati kwa Uwekezaji ikiwemo ukaribu Jiji la Dar es salaam, Uwepo wa Miundombinu muhimu kwa Uwekezaji ikiwemo Reli ya kisasa ya Mwendokasi SGR, Umeme na Maji kutosha na uwepo Kongani kubwa ya Viwanda Baran Afrika ya Sino Tan Kwala Industrial Park.”alisisitiza.
Naye Balozi Ameeleza kuwa amefika na Mwekezaji huyo kuona Fursa ya Kuwekeza kwenye Machinjio ya kisasa, Unenepeshaji Mifugo, Chakula cha Mifugo, Kilimo cha kisasa, Viwanda vya Vifungashio na Uwekezaji kwenye Sekta ya Uvuvi.
Hata hivyo, Kunenge amemhakikishia kwamba Ardhi ya uhakika ipo kwa ajili ya Uwekezaji huo.
“Baada ya Mazungumzo yetu mnatembelea Eneo la Chalinze Chamakweza na Visegese Kisarawe kuona Ardhi hiyo na Baadae mtapatembelea Rufiji na Kibiti kuona Fursa katika Kilimo”Ameeleza Kunenge.