Mkurugenzi wa Medala High school Emmanuel Mfikwa akiongea na waandishi wa habari ambao walikuwa wamefika shuleni hapo wakati wakiendelea na ziara ya Iringa Journalist’s Ruaha The Royal Tour na kuongea na mkurugenzi huyo aliyeunga mkono ziara hiyo ya kutangaza na kutembelea hifadhi ya Ruaha.Mkurugenzi wa Medala High school Emmanuel Mfikwa akiongea na waandishi wa habari ambao walikuwa wamefika shuleni hapo wakati wakiendelea na ziara ya Iringa Journalist’s Ruaha The Royal Tour na kuongea na mkurugenzi huyo aliyeunga mkono ziara hiyo ya kutangaza na kutembelea hifadhi ya Ruaha.Baadhi ya wanafunzi wa Medala High School wakiwa kwenye picha ya Pamoja Mbele ya Jengo la Utawala la shule hiyoMuonekano wa juu wa Majengo ya Medala High School
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Uongozi wa Medala High school iliyopo mkoani Iringa imeunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutangaza utalii wa kutembea hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa walipotembelea shule ya Medala iliyopo tarafa ya Idodi wakati wakiwa kwenye ziara ya Iringa Journalist’s Ruaha The Royal Tour, mkurugenzi wa Medala High school Emmanuel Mfikwa alisema kuwa ameamua kuunga mkono juhudi za waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa kwa kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Mfikwa alisema kuwa anatambua mchango wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo inapambana kuvitangaza vivutio vilivyopo nchini kwa njia mbalimbali ikiwemo filamu ya Royal Tour ambayo imeigizwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivyo kitendo cha waandishi wa habari Iringa kutembelea hifadhi hiyo kunaongeza chachu ya kukuza utalii wa ndani.
aliongeza kuwa uongozi wa Medala High School kwa ushirikiano na mkurugenzi walitoa katoni kadhaa za maji ya kunywa na kiasi cha fedha kwa ajili ya waandishi wa habari kujikimu wakati wanafanya utalii na kuanda habari za kuitangaza hifadhi ya taifa ya Ruaha.
Alisema kuwa Medala High school iliyopo kata ya Idodi wilaya ya Iringa imekuwa na utaratibu wa kuwapeleka wanafunzi wa shule hiyo mara kwa mara kwenda kutalii katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha na wamepanga kuwapeleka wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika hifadhi hiyo kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii.
Mfikwa alisema kuwa wanafunzi wa Medala High school wamekuwa wanafundishwa kwa ubora ambao unatakiwa na kuwafundisha uzalendo wa kutembelea hifadhi na vivutio vilivyopo nchini kwa kuwajengea uwezo wa kupenda kwenda kutalii.
Aidha mkurugenzi wa Medala High school Mfikwa alisema kuwa malengo ya shule hiyo ni kutoa elimu ilivyo bora kwa wanafunzi ambao watakuwa wanasoma hapo kwa kuajili walimu na wafanyakazi wenye taaluma inavyotakiwa kila idara ili kuhakikisha Wanafunzi akitoka hapo anakuwa bora kila eneo.
Alisema kuwa wanampango wa kuajili walimu wenye ubora kutoka pande zote za Africa Mashariki ili mradi awe amefikia ubora wa kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa shule hiyo kama ambavyo walimu waliopo wanavyofanya hivi Sasa.
“Waandishi wa habari angalieni hili shule inamazingira yaliyo bora na tulivu kumpa kumuwezesha mwanafunzi kusoma akiwa huru kwa kuwa mahitaji yote muhimu yanapatika hapo shuleni kwa wakati hivyo si dhani kama Kuna mzazi atakataa mtoto wake asisome katika shule yangu ya Medala High school”alisema Mfikwa
Mfikwa alisema kuwa Medala High school inapokea wanafunzi wa bweni kutoka na mazingira shule iliyopo na lengo ni kuhakikisha wanatoa elimu iliyo bora na kufanya mapinduzi ya kitaaluma kwa shule zilizopo mkoa wa Iringa na nje ya Iringa kwa namna ambavyo amekuwa na walimu bora na nguli wa kutoa elimu bora kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.
Mkurugenzi wa Medala High school alimazia kwa kusema kuwa wamekuwa wakiwasomesha bure baadhi ya wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye mtihani wa kidato cha nne na darasa la saba wanaotoka katika kata ya Idodi na tarafa ya Idodi kwa ujumla huku lengo kubwa likiwa ni kukuza elimu ya wananchi wa eneo hilo ambao asili yao kubwa ni wafugaji.
Medala High school inapatikana mkoani Iringa wilaya ya Iringa kata ya Idodi karibu na hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambapo unaweza kuwapigia kwa namba hizi hapa 0736313180,0715817236,0678122682,0713961069 na 0758313180 muda wote wanapatikana.
Kwa upande wao baadhi ya waandishi wa habari Iringa walimpongeza mkurugenzi wa Medala High school kwa uwekezaji ambao unatija kwa maendeleo ya elimu kwa wananchi wa Tanzania kutokana mazingira yalivyojengwa kwa ubora unatakiwa.
Walisema kuwa wamevutiwa na mazingira ya Medala High school na watakuwa mabalozi wa shule hiyo ya bweni ambayo inamajengo yanayotakiwa na kuliziwa na mzazi yoyote yule kumpeleka mtoto wake akasome katika shule hiyo.
Waandishi wa habari walimalizia kwa kumshukuru mkurugenzi wa Medala High school na wafanyakazi wote kwa mchango wao kufanikisha ziara ya Iringa Journalist’s Ruaha The Royal Tour ambayo ilikuwa na lengo la kwenda kutalii na kuendelea kuitangaza hifadhi ya Taifa ya Ruaha.