Na. Abel Paul wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha.
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha kupitia kikosi cha usalama Barabarani mkoa wa Arusha kimetoa elimu kwa madereva Zaidi ya mia moja (100) na kimewakumbusha madereva wa mabasi yaendayo mikoani kutii sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali kama sio kumaliza kabisha ajali za barabarani katika mkoa wa Arusha.
Hayo yamesemwa leo agosti 16 2022 na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha mrakibu wa Polisi SP SOLOMON MWANGAMILO katika stand kuu ya mabasi yaendayo mikoani na nchi Jirani ambapo amesema kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha kimejipanga vyema kudhibiti ajali katika mkoa wa Arusha.
Mwangamilo amesema kuwa ajali nyingi zimekuwa zikisababishwa na mwendokasi pamoja na kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari (overtaking) ambapo ameeleza kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikiacha simanzi kwa familia,ndugu na jamaa ambao upoteza wapendwa wao kwa uzembe wa baadhi ya madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani.
SP Mwangamilo ameeleza kuwa katika siku za hivi karibu kumejitokeza tabia ya madereva kukiuka taratibu nasheria za usalama barabarani na kuendesha magari hayo mwendo kasi ambapo amesema kuwa dereva atakaye kamatwa akikiuka sheria hizo atakamatwa na kufungiwa leseni yake kwa kipindi cha miezi mitatu hadi sita.
Nao baadhi ya madereva wa mabasi yaendayo mikoani wamelishukuru Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha hususani kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha kuendelea kutoa elimu kwa madereva mara kwa mara ili kuwajengea uwezo na umahiri ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika.