Mwenyekiti wa kamati ya Sensa Wilaya ya Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na Makarani, Maudhui na watu wa Tehama wa Sensa ya watu Makazi wilayani humo kutanguliza uzalendo katika utekelezaji wa zoezi la SENSA la kitaifa

Na Fredy
Mgunda,Iringa.
Mwenyekiti wa kamati
ya Sensa Wilaya ya Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan
Moyo amewataka Makarani, Maudhui na watu wa Tehama wa Sensa ya watu Makazi
wilayani humo kutanguliza uzalendo katika utekelezaji wa zoezi la SENSA
la kitaifa ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo iliyoyakusudia ya kuwahesabu
watu kama ambavyo inatakiwa kuwa Mwaka huu.
Akizungumza na
Makarani, Maudhui na watu wa Tehama wa Sensa wanaoendelea na mafunzo katika
Manispaa ya Iringa Moyo alisema kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi ili
kufanikisha zoezi hilo muhumu litakalosaidia upangaji wa bajeti sahihi ili
kuiwezesha kufikisha huduma za msingi katika Kila Kona ya nchi hivyo ni muhumu
watu waliopewa dhamana ya kutekeleza zoezi hilo wakalitekeleza kikamilifu na kwa
weledi wa hali ya juu.
Moyo aliwataka
wahusika wa zoezi la Sensa kuhakikisha wanatunza Siri za taarifa za watu
watakaowahesabu ikiwa ni pamoja na utunzaji wa vitendea
walivyopatiwa na Serikali katika kutekeleza zoezi Hilo.
Alisema kuwa mhusika
yeyeto yule wa zoezi la Sensa atakayepoteva au kuvuruga zoezi la Sensa serikali
itamchulia hatua kali za kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi,hivyo kila
mhusika anatakiwa kuwa makini na zoezi hilo la kitaifa kwa manufaa ya nchi ya
Tanzania.
Aidha Mohamed Moyo
amewaonya Makarani hao pamoja na Watu Wote watakaobainika kuzembea katika
utekelezaji wa jukumu walivyopatiwa na Serikali ikiwemo watu Wote
wanakajihusisha na uhujumu Kwa lengo la kukwamisha shughuli za Sensa
itakayifanyika Rasmi Agosti 23 mwaa huu.
Akifafanua zaidi
amewataka Wananchi kuwa Tayari kwani kuanza Tarehe 21 Hadi 22
Agosti Mwaka huu Karani wa Sensa akiongozwa na kiongozi wa eneo husika atafika
kwenye eneo alilopangiwa kujitambulisha na kutambua mipaka ya eneo lake hivyo
Kila Mwananchi awe Tayari kutoa ushirikiano Ili kufanikisha zoezi Hilo.
Moyo alimazia kwa
kuwaomba wananchi wa wilaya ya Iringa kuhakikisha wanahamasishana kujitokeza
kuhesabiwa siku ya zoezi la Sensa kwa ajili ya manufaa yao na serikali kujua
namna gani ya kupanga bajeti ya eneo husiku kupitia SENSA hiyo ya mwaka huu.